TIMU ya
Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeifunga Harambee Stars ya Kenya bao
moja kwa sifuri. Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na
FIFA imefanyika leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Vijana wa
Stars ya Tanzania leo wametoa burudani nzuri kwa wakazi wa Jiji la
Mwanza na viunga vyake ikiwa ni kukidhi kilio cha muda mrefu cha kuomba
mikoa ya Kanda ya Ziwa ipate nafasi ya kuishuhudia timu ya Taifa ‘Taifa
Stars’ ikivaana na timu ya nje.
Wapenzi
wa soka wa Kanda ya Ziwa mara kwa mara wamekuwa wakilitupia lawama
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa linawanyima nafasi ya kushuhudia
mechi za Taifa Stars kwa kuwa mechi nyingi zinafanyika Dar es Salaam au
mikoa ya jirani.
No comments:
Post a Comment