EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, December 15, 2012

THEA AANIKA USHOGA, UMALAYA ,UKUWADI NA USAGAJI NDANI YA BONGO MOVIES.

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
Kufuatia kugubikwa na skendo lukuki zikiwemo ushoga, umalaya, ukuwadi, usagaji na uchafu wa kila aina ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo (Bongo Movies), staa ‘legendary’ wa kiwanda hicho, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ ameanika kuwa mambo hayo ndiyo yanayowaharibia kazi zao kwenye jamii.
 
Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’
Thea mwenye takribani miaka 10 ndani ya sanaa hiyo aliiambia Funguka na Risasi Jumamosi kuwa kwa sasa tasnia ya filamu za Kibongo imechafuka kwa skendo tofauti na ilivyokuwa zamani.
Alisema kuwa yanayofanyika ni aibu hata kwa wasanii kujiita kioo cha jamii hivyo kuomba asionekane mbaya kwa kusema ukweli kwa nia njema tu .

 
Risasi: Unafikiri ni nini sababu ya tasnia ya filamu kugeuka kichaka cha kufanyia uovu tofauti na ilivyokuwa zamani?
Thea: Sababu kubwa ni wasanii wanaoingia kwenye tasnia bila kujua maadili ya uigizaji na utaratibu wake kwani ukiangalia wanaofanya uchafu huo hawajapitia kwenye vikundi vya sanaa na hawajui maana ya uigizaji.
Risasi: Mbali na wasanii ambao hawajapita kwenye vikundi, wapo pia waliopitia huko (kwenye vikundi vya sanaa) lakini nao wanatajwa kwenye skendo za usagaji na ushoga. Hili unalionaje?
 
Thea: Ni kweli wapo baadhi wanaofanya hivyo na ukweli ni kwamba hawa kaka zetu wanatutia aibu sana na kinachowaponza ni tamaa za kutaka mafanikio ya haraka. Hawajui kuwa Mungu amempangia kila mtu riziki yake, matokeo yake wanafanya uchafu ili waonekane wana magari ya kifahari.
Risasi: Unalizungumziaje suala la ushirikina kwenye tasnia ya filamu kwani waigizaji wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanalogwa na wengine wakionekana wanakuja juu kwa kasi hivyo kuhusishwa na ulozi?
Thea: Nimesikia habari hizo lakini mimi siamini uchawi na hakuna anayeweza kuniloga kwa sababu nina Yesu ambaye hakuna linaloshindikana kwake.
 

Risasi: Je, unazungumziaje hili la waigizaji ambao wanatajwa kujihusisha na ushirikina na wanakuja juu kwa kasi?
Thea: Jamani wasanii wenzangu kama mnafanya hivyo acheni na tukubali mabadiliko kwenye sanaa kwani kila siku vinazaliwa vizazi vipya kwa hiyo kila mtu ana wakati wake wa kupanda.
Risasi: Vipi kuhusu skendo ya umalaya iliyoshamiri kwa wasanii wa kike ndani ya tasnia ya filamu?
Thea: Ni kweli wasanii wa filamu ni malaya sana na asilimia 90 ya waigizaji wa kike wapya ndiyo wanaoongoza kwa kuchafua tasnia kwani kila uchafu uko ndani ya filamu. Mara kukaa utupu, ukuwadi, kugombea mabwana na mengine mengi yasiyopendeza mbele ya jamii.
Risasi: Ni kitu gani kifanyike ili kuondokana na uchafu wote huo?
Thea: Nawashauri wamuombe Mungu sana na waachane na maisha ya kuiga na kutamani vitu ambavyo hawawezi kuvipata. Wasanii wafanye kazi kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.
Risasi: Tofauti na skendo ulizozungumzia, pia kuna suala la wasanii kujitenga makundi-makundi, hili likoje?
Thea: Sitaki kulisemea sana hilo kwa sababu Tanzania ilipiganiwa na watu wachache mpaka tukapata uhuru hivyo tasnia ya filamu nayo itapiganiwa na wasanii wachache na taratibu tutafika kwenye usemi na lugha moja.
Risasi: Baada ya kuwaona wasanii wakifanya mambo machafu huwa unawasaidiaje ukiwa kama mwigizaji mkongwe?
Thea: Sina cha kuwasaidia kwa sababu katika kuingia kwenye filamu kuna watu waliwashika mkono na kuwasaidia hivyo haohao wanatakiwa kuwasaidia kimawazo na ushauri ili wabadilike lakini wao ndiyo wanawafanya mabibi na mabwana zao, mimi wale niliowasaidia lazima niwafundishe maadili ya uigizaji.
Risasi: Hivi sasa wakongwe mmekuwa kimya sana na mnaonekana kupitwa na wasanii wapya wanaoingia kwenye filamu, kwako hili unalionaje?
Thea: Unajua pumba na mazao huwa vinajitenga, wapo wasanii wanaoingia na kuwika sana lakini hawadumu, wanapotea kwa muda mfupi.
Risasi: Je, umejipanga vipi kukabiliana na changamoto za wasanii chipukizi?
Thea: Kila kazi ina changamoto zake kwa sababu zamani tulibweteka kwani tulikuwa wachache ila mpaka sasa sijaona mtu wa kunitisha kwa wanaokuja.CHANZO CHA HABARINAGAZETI LA RISASI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate