Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa wapiganaji
wote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kuacha mapigano
kwa ajili ya kuthamini ubinaadamu.
Ban ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukusanya fedha
kiasi bilioni 1.5 kwa ajili ya wakimbizi wasyria, unaofanyika nchini
Kuwait. Amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa zaidi ya wasyria milioni 4
wanahitaji msaada wa dharura,na kwamba raia wa kawaida wanateseka
kupita kiasi, hivyo wanahitaji kupatiwa msaada sahihi. Umoja wa Mataifa
unapanga kuwapatia mahitaji ya msingi raia milioni 4 waliyoko ndani ya
Syria, na zaidi ya wakimbizi 650,000 waliyoyakimbia makaazi yao kutokana
na mgogoro huo unaokaribia miaka miwili.
Mfalme wa Kuwait, Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.
Kuwait yatoa dola milioni 300
Wawakilishi kutoka mataifa zaidi ya 60 wanahudhuria mkutano huo wa
kimataifa kusikia maombi ya Umoja wa Mataifa ya kuchangisha dola bilioni
1.5. Maafisa wa umoja huo wanasema wana kiasi kidogo tu cha fedha
zinazohitajika, ingawa ahadi kutoka mataifa na mashirika mbalimbali
ziliongezeka kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Umoja wa Ulaya na marekani
ziliahidi kutoa jumla ya dola milioni 400.
Mfalme wa Kuwait Sheikh Sabah al-Ahmad al-Saba, naye ametangaza leo kuwa
atachangia dola milioni 300. Sheikh al-Saba ameuambia mkutano huo kuwa
taarifa za kutisha juu ya vurugu zinazoendelea nchini Syria,zinazua
maswal ijuu ya mustakabali wa Syria, na kuongeza kuwa juhudi za msaada
zinapaswa kuongezwa mara mbili. Umoja wa Falmeza Kiarabu nao ulitarajiwa
kutoa kiasi cha dolamilioni 300.
Brahimi alitaka baraza la usalama kuchukua hatua sasa
Mjumbe wa kimataifa wa amani katika mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi
alisema vita nchini Syria vimefikia kiwango cha kutisha ambacho
hakijawahi kushuhudiwa, baada ya wanaume kadhaa kukutwa wakiwa
wamechinjwa. Brahimi aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
jana Jumanne, kuwa linapaswa kuchukua hatua sasa hivi kukomesha mauaji
ya kutisha, kama yanayoshuhudiwa hivi sasa ikiwa ni pamoja na yale ya
wanaume wasiyopungua 78, kilamoja wao akiwa ameuawa kwa kupigwa risasi
moja na kisha kutupwa mtoni katika mji wa Aleppo.
Mama akimshika mtoto wake aliyejeruhiwa akisubiri matibabu katika hospitali nchini Syria.
Baada ya miezi 22 tangu kuanza kwa mgogoro huo, watu zaidi ya elfu 60
wameuawa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.Brahimi alisema uhalali wa
utawala wa Assad umeharibika kabisaa kiasi cha kutokarabatika,lakini
alionya kuwa bado unaweza kuendelea kun'gan'gania madarakani. Brahimi
alisema vikosi vya serikali na waasi wote wanatenda uhalifu katika
mgogoro huo.
Baraza la usalama bado limegawanyika
Lakini balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Suzan Rice, alisema
masuala ambayo yamekuwa yakiligawa baraza la usalama yameendelea kuwepo
na hivyo hakuna njia rahisi ya kusonga mbele.Baraza la usalama la Umoja
wa Mataifa limekabiliwa na mkwano juu ya Syria kwa zaidi ya mwaka
moja.Urusu na China zimetilia guu maazimio matatu ya Baraza hilo
yaliolenga kulaani ukandamizaji unaofanywa na utawala wa rais Assad.
Urusi inazishtumu nchi za magharibi kwa kutaka kubadilisha utawala
nchini Syria kwa nguvu,na inasisitiza kuwa haiwezi kumlaazimisha Assad
kuachia madaraka. Marekani na washirika wake wanaunga mkono msimamo wa
upinzani,kuwa hakuwezi kuwa na mazungumzona Assad.
No comments:
Post a Comment