Mwezi mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini Kenya bado kuna wasiwasi juu ya maswala mengi huko hasa usalama.

Kulingana na wanaharakati nchini humo bado wanasiasa wanaendelea kueneza
siasa za chuki na za kikabila maswala ambayo ni tete na ndio
yaliosababisha ghasia za baada ya uchaguzi miaka mitano iliopita.
Uchaguzi nchini Kenya unatarajiwa kufanyika taraehe 4 mwezi ujao.
Professa Tom Namwamba ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa nchini Kenya,
na Amina Abubakar amezungumza naye muda mfupi uliopita na kwanza
anaelezea hali halisi nchini Kenya kwa sasa
No comments:
Post a Comment