EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, February 8, 2013

Hoja ya Mbatia yatupwa

SUALA la mitalaa ya elimu nchini limeibuka tena bungeni jana baada ya mtoa hoja, James Mbatia kusema hakubaliani na mitalaa iliyowasilishwa kwa Spika kama kielelezo cha kuwepo kwake.
 
Juzi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliwasilisha mitalaa ya elimu kama alivyodai Mbatia baada ya kuwasilisha hoja binafsi iliyozungumzia udhaifu wa elimu.

Hata hivyo, kabla ya kuthibitishwa na Bunge, Naibu Spika, Job Ndugai aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake.

Kamati hiyo iliyopewa kazi ya siku moja, ilikuwa chini ya mwenyekiti wake, Magreth Sitta pamoja na Mbatia mwenyewe. Wajumbe wengine wa kamati ni Benadetha Mshashu, Abdul Jabil, Khalifa Khalifa, Yahaya Kassim Issa na Israel Natse.

Akiwasilisha taarifa ya kamati bungeni jana, Spika wa Bunge, Anna Makinda alisema:
“Baada ya Serikali kuwasilisha mitalaa ili kujiridhisha, iliunda kamati kuchunguza ukweli wa mitalaa hiyo.

“Baada ya kukabidhiwa nyaraka mbalimbali kuhusiana na hilo, kamati iliwasilisha taarifa yake ya kuthibitisha kuwa mitalaa hiyo ilikuwa halali na sahihi na ninaagiza igawiwe kwa wabunge,” alisema Makinda kabla ya kuahirisha Bunge.

Baada ya hoja ya Spika, Mbatia aliomba mwongozo wa Spika na alipopewa nafasi alisema: “Kwa mujibu wa Kanuni 37 (4), baada ya hati kuwasilishwa, Mwanasheria Mkuu ana wajibu wa kuwasilisha taarifa ya kutaka hoja ijadiliwe.

Mbatia atoa ufafanuzi
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kutoka katika Ukumbi wa Bunge, Mbatia alisema kuwa hakubaliani na mitalaa iliyowasilishwa ambayo ni ya elimu ya awali, msingi na sekondari.

Alisema kilichowasilishwa siyo alichokidai bungeni, mtalaa alioudai ulikuwa wa mwaka 1997 hadi mwaka 2005 wakati uliowasilishwa ni wa mwaka 1998 hadi 2008 ambao unasema ni kwa ajili ya Tanzania Bara.

“Huwezi kusema Mtalaa wa Elimu ya Sekondari ni wa Tanzania wakati huu uliopo unaonyesha ni wa Tanzania Bara wakati hata mtihani unaofanyika wa darasa la saba ni wa Tanzania.

“Kasoro nyingine ni kwamba katika vitabu vya mwongozo inatakiwa kuwa na Alama Ubora (ISBN) kwa kuidhinishwa na Bodi ya Maktaba, sasa mtalaa wa jana hauna hayo yote.”
Kasoro ya tatu, Mbatia alisema alikataa muhtasari kwa kuwa haukuwa na saini ya Kamishna wa Elimu.
Alisema kuwa bado anasimamia hoja yake kuwa hakuna mitalaa ya elimu Tanzania na atasimamia hapo na atamwomba Spika suala hilo lijadiliwe na Wabunge wote kwa masilahi ya taifa, kwani mtalaa wa taifa hauwezi kutolewa kwa waraka.
Kawambwa azungumza
Akijibu hoja za Mbatia, Waziri wa Elimu, Shukuru Kawambwa alisema; Suala la kuweka alama ya ubora, halina mashiko kwa kuwa hutolewa kwa machapisho ya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, alisema suala hilo linasimamiwa na maktaba kuu.
“Mimi ninachotaka kusema, mitalaa iliyowasilishwa ndiyo hiyo na Kamati imemsaidia Spika kumweleza na kumhakikishia hili, nimesikitika sana na hoja zake kuwa zinataka kupotosha na naweza kusema vielelezo alivyotoa ni feki.

“Tuko makini, tunawajali wananchi na hili la kusema elimu ya Tanzania Bara na Tanzania ni makosa tu ya uchapaji,” alisema Kawambwa.

Mvutano ndani ya Kamati
Akizungumzia suala hilo baadaye jana, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Israel Natse alisema ilikuwa vigumu kupitisha mitalaa hiyo ambayo hata wajumbe wa kamati walikiri baadhi ya hoja za Mbatia zilikuwa za ukweli.

“Kulikuwa na mvutano mkubwa, wajumbe wenyewe walikiri makosa, lakini kama unavyojua, kila upande ulikuwa unavutia kwake na kikubwa ni kwamba kulikuwa na mitalaa, lakini kutolewa kwake ilikuwa ikitolewa kwa waraka.

“Kuna maeneo tuliwabana wahusika wakakiri, lakini tulikubaliana kuwa iwasilishwe hivyohivyo na zaidi ni kwamba kilichowasilishwa sicho, kwani ilitakiwa mitalaa ya mwaka 1997 hadi mwaka 2005 wakati kilicholetwa ni mitalaa ya mwaka 1998 hadi mwaka 2008 ambayo hata kwenye ‘hansard’ haipo.
                                               CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate