EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, March 5, 2013

Mahakama:Ponda, wenzake 49 wana kesi ya kujibu

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Victoria Nongwa amesema Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote matano yanayowakabili.
 
Sheikh Ponda Issa Ponda akipunga mkono wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mahakama hiyo kumuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka yake, jijini Dar es Salaam jana
Sheikh Ponda na wenzake hao wanakabiliwa na mashtaka matano, likiwamo la kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni, uchochezi na kuingia  katika ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Limited kwa nia ya kujimilikisha visivyo halali.

Akitangaza uamuzi huo, Hakimu Nongwa alisema: “Mahakama imepitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa upande wa mashtaka... inaonekana wazi shauri hili linatokana na kipande cha ardhi.”


Kiongozi huyo na wenzake wanatarajiwa kuanza kujitetea Jumatano na Alhamisi.
Hakimu Nongwa alieleza kuwa baada ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), kubadilisha ardhi ya ekari nne zilizopo Chang’ombe Markazi na 40 za Kampuni ya Agritanza Ltd zilizopo Kisarawe, kuna baadhi ya Waislamu hawakuridhika.

Alisema Mahakama haitaujadili kwa undani ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, bali itawapa nafasi upande wa utetezi kujitetea... “Kila mshtakiwa anatakiwa aseme alikuwa anatafuta nini katika maeneo yale ya Chang’ombe Markazi.,”
Alisema kabla ya Sheikh Ponda na wenzake kuanza  kujitetea, Wakili wao Juma Nassor anatakiwa apeleke vielelezo watakavyovitumia na kueleza watatoa utetezi kwa njia ya kiapo ama la.

Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda, Saleh Mukadam na wenzao 48, wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwamo la wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.
Mbali na mashtaka hayo, pia Ponda na Mukadam wanakabiliwa na shtaka la uchochezi ikidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka huu katika eneo la Chang’ombe  Markazi, wakiwa viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, waliwashawishi wafuasi wao kutenda makosa hayo.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka alisema Oktoba 12, mwaka huu katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Temeke, kwa jinai na pasipo sababu za msingi walivamia ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.
Kweka alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo la kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa, kinyume na Kifungu cha 85 na 35 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai kuwa kati ya Oktoba 21 na 16, mwaka huu katika eneo hilohilo, washtakiwa hao pasipo uhalali wowote na hali iliyosababisha uvunjifu wa amani, walijimilikisha ardhi hiyo mali ya Agritanza Limited.

Aidha Hakimu Nongwa alisema washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vifaa na malighafi mbalimbali za ujenzi, yakiwamo matofali 1500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh 59,650,000, mali ya Kampuni ya Agritanza Ltd, kati ya Oktoba 12 na 16.
Awali, baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka  yanayowakabili kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha hati za kuzuia dhamana zao chini ya Kifungu cha 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA).
Mara ya kwanza kesi hiyo ilifika Mahakama ya Kisutu Oktoba 18 na tangu wakati huo ilikuwa ikisikiliza mashahidi upande wa utetezi na kabla ya kufikia uamuzi huo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate