
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ameruhusiwa
kwenda nyumbani baada ya kupata matibabu katika hospitali moja mjini
Pretoria. Madiba mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini mwishoni
mwa wiki kwa ajili ya vipimo vya afya yake.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alisema Jumapili kwamba madaktari
wamekamilisha vipimo vyote vilivyokuwa vimepangwa na kwamba Bw. Mandela
yupo kwenye hali nzuri na ilivyokuwa siku za nyuma, afya yake inaendelea
kuangaliwa na timu ya madaktari.
Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj amesema hakuna sababu
yeyote ya kuwa na wasiwasi wakati madaktari wakiendelea kumfanyia
uchunguzi zaidi mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel. Bw. Mandela
alilazwa mwezi Desemba kwa sababu ya maambukizo kwenye mapafu.Chanzo cha habari hidhaa ya kiswahili irani
No comments:
Post a Comment