EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, March 3, 2013

MBIO ZA VODACOM ZANOGESHA MSIMU WA KILIMANJARO MARATHON

Mmoja wa washiriki wa mbio za kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run" Bw. Moses Msaka (katikati) akimalizia mbio zake. Mmasai huyo alivutia washiriki wengi wa mbio hizo kwa kukimbia akiwa amevalia nguo zake za kawaida.
Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Bw.Ibrahim Kaude akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mbio za kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run".

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Rukia Mtingwa pamoja na mfanyakazi mwenzake wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run".

Watoto Francis Ngowi (kushoto) na Moses John wote wenye umri wa miaka 14 wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run" ambazo ni sehemu ya  mbio ndefu za Kilimanjaro Marathon.

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishangilia kwa kumaliza mbio za kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run" ambazo ni sehemu ya mbio ndefu za Kilimanjaro Marathon.

Baadhi ya washiriki wa mbio kujifurahisha za "Vodacom 5 KM Fun Run" wakishiriki katika mbio hizo ambazo ni sehemu ya mbio ndefu za Kilimanjaro Marathon.


MBIO ZA VODACOM ZANOGESHA MSIMU WA KILIMANJARO MARATHON

  • ZAVUTIA ZAIDI YA WAKIMBIAJI 7,000
  • WAKIMBIAJI WOTE WAPATA ZAWADI YA USHIRIKI KUTOKA VODACOM
Maelfu ya wakazi wa Mji wa Moshi na vitongoji vyake ikiwemo wageni mbalimbali kutoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na wa nje ya nchi wameshiriki mbio za kujifurahisha za Kilomita Tano za Vodacom zijulikanazo kama "Vodacom 5 KM Fun Run" zinazofanyika pembezoni mwa mbio za Nyika za Kilimanjaro.
Katika mbio hizo zinazofadhiliwa na kampuni ya mawasiliano Vodacom zimevutia wakimbiaji zaidi ya 7,000 na hivyo kuendelea kuwaza kipekee kwa jinsi inavyotoa nafasi kwa makundi mbalimbali kushiriki kama sehemu ya kusherehekea msimu wa mbio za kila mwaka za Kilimanjaro Marathon.
Kupitia mbio hizo za kujifurahisha za Vodacom makundi mbalimbali ya wasio wakimbiaji wa kulipwa yaani 'Proffessional Runners hupata fursa ya kushiriki na kuwa sehemu ya shamrashamra za Kilimanjaro Marathon na pia kutumia nafasi hiyo kunyoosha viungo, kuimarisha afya huku wengine wakitumia mbio hizo kama kipimo cha kujipanga kushiriki mbio ndefu katika mashindano mbalimbali.
Mbio hizo zilianzia eneo la Nje ya Chuo Kikuu cha Ushirika cha Mjini Moshi zikianzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ibrahim Msengi na kumalizikia ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Chuo hicho ambapo washiriki walipata zawadi mbalimbali za ushiriki kutoka kampuni ya Vodacom.
Akizungumzia mbio hizo, Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom, Ibrahim Kaude amesema Vodacom inajivunia kuwezesha kila mmoja kuwa sehemu ya mbio za Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka.
“Kila Mtanzania na hata asie Mtanzania hususan wasio wakimbiaji wa kulipwa angependa kuwa sehemu ya tukio hili kubwa lenye mvuto na sura ya kimataifa hivyo kwetu sisi kuwezesha hilo ni jambo tunalolifurahia na kulipa kipaumbele kila mwaka.” Amesema Kaude
 

Kaude amesema katika kuonesha kuwa mbio hizo ni za kipekee na zinafurahiwa na kila mmoja idadi ya washiriki imeongezeka kwa kiasi kikubwa kulinganisha na idadi ya walioshiriki mbio hizo mwaka jana.
Pamoja na kubeba jina la mbio za kujifurahisha lakini mbio hizo zimeonekana kuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa washiriki miongoni mwao wakiwa wanafunzi wa shule mbalimbali, taasisi, mashirika ya kitaifa na kimataifa pamoja na wakimbiaji mmojammoja.
 

Katika kuhakikisha kila mmoja anakuwa sehemu ya mbio hizo baadhi ya watu wameonekana wakikimbia na watoto wao huku wakiwahamasisha kuhakikisha wanamaliza mbio hizo ambapo mshindi wa kwanza alitumia kiasi cha dakika 20.
Kwa upande wa washindi wanaume, Bw. DotoI Kangaa alishika nafasi ya kwanza na Elibariki Buko nafasi ya pili wamesema pamoja na kwamba mbio hizo ni za kujifurahisha bado zimekuwa na ugumu kwa kuwa idadi ya washiriki wenye uwezo wa kukimbia ni kubwa na hivyo kutoa ushindani.
 

Hata hivyo washindi hao wameipongeza Vodacom kwa kutengeneza mazingira ambayo kila mmoja ana kuwa na nafasi ya kufurahia msimu wa Kilimanjaro Marathon na hivyo kulifanya tukio hilo kuwa na sura halisi ya Kitanzania kwa kuwa kinyume cha hapo ingeshuhudiwa idadi kubwa ya wakimbiaji wa nje wakishiriki katika mbio ndefu.
Mbio hizo zimetoa washindi watano ambao wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu zikiwa na jumla ya thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni Tisa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate