Wakenya waanza kupiga kura
Raia wa Kenya wameanza shughuli ya kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza unaofanyika chini ya katiba mpya.
Katika uchaguzi huu watamchagua rais pamoja na wawakilishi wa wanawake, magavana, na maseneta wa majimbo 47 ya nchi hiyo.Katika mji mkuu Nairobi misururu mirefu ya
wapigakura ilionekana kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa 12 za
Afrika mashariki.
Ushindani mkubwa wa kiti cha urais unatarajiwa
kuwa baina ya kiongozi wa muungano wa Cord, Raila Odinga, na yule wa
muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta.
No comments:
Post a Comment