Zaidi ya raiya mia moja na
themanini na tano wamefariki huku nyumba elfu mbili zikiharibiwa
kutokana na mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Kiislamu
kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole.
Jeshi na maafisa wa serikali
wanasema kuwa kulikuwa na mashambulizi ya gurunedi, zilizosukumwa na
roketi na makabiliano ya risasi katika mji tulivu wa Baga unaopakana na
Chard Ijumaa jioni.
Wakazi walikimbili misituni na kurejea hapo jana
ila walipata sehemu kubwa ya mji huo imeharibiwa na maiti na mizoga
ikiwa imetapakaa kila mahali.
Mwanahabari mmoja amesema kuwa hali hiyo
inadhirisha namna mapigano yamezidi Nigeria katika eneo la Kasikazini
ambalo lina waislamu wengi.
Alisema wapiganaji walikuwa na silaha nzito
kuliko zilizotumika katika mashambulizi ya hapo awali katika eneo hilo
nao manusura wanasema washambuliaji wengi walikuwa wakizungumza lugha ya
kigeni.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea.
Brigedia Jenarali Austin Edokpaye amewaambia
maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na
maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji
hao walikuwa wakitumia raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na
makaazi ya watu ambapo walijua vikosi vya jeshi visingeweza kujibu
mapigo.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na vifo vya raia
wengi tangu kuibuka kwa vikundi vya wapiganaji wa kiislamu mwaka 2010
ambapo vingi vimejikita Kaskazini mwa nchi hiyo.
CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment