EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, April 20, 2013

Azam ushindi mbele kwa mbele leo

Azam FC inafahamu kwamba ina fursa kujisafishia njia ya kucheza hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini hilo litawezekana ikiwa itaibuka na ushindi leo dhidi ya timu imara ya maafande wa FAR ya Morocco.


Mtanange huo baina ya wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa na Waarabu hao litapigwa kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam inayohaha kutaka kuandika historia mpya ya michuano hiyo licha ya kwamba inashiriki kwa mara ya kwanza, itaingia uwanjani ikijivunia kasi yake ya kuridhisha katika mechi zilizotangulia.

Matokeo ya ushindi wa jumla ya mabao 8-1 dhidi ya Al Nasri ya Sudan Kusini, kisha ule wa mabao 2-1 dhidi ya Barack Young Controller II ya Liberia ni wazi yatatumiwa kama kichocheo cha kuizamisha FAR leo.
Kocha wa Azam Stewart Hall amewataka washambuliaji wake wahakikishe wanatumia nafasi kikamilifu kwa kufunga mabao kadri inavyowezekana.

Pamoja na hilo, Hall amewataka mabeki wake wawe makini ili waweze kuepusha madhara yanayoweza kuikabili timu yake kutokana na mashambulizi ya kushtukiza ya FAR.
“Sisi tutacheza mfumo wetu ule ule wa 4-4-2, tukimiliki mpira muda mwingi na kufanya mashambulizi ya kusaka mabao kwa tahadhari tukijihami na mbinu ya wapinzani wetu kutushambulia kwa ghafla,” alisema Hall.


Hall huenda akampumzisha mshambuliaji Brian Umony ambaye kwa mujibu wa mazoezi ya timu hiyo anaonekana kutokuwa fiti licha ya kwamba alicheza mechi dhidi ya Barrack.
Naye kocha wa FAR Ouadani Lahcen amesema hana ufahamu wa kutosha na Azam, lakini yuko tayari kuikabili na kuvuna ushindi akitumia mbinu ‘alizoiba’ kutoka Timu ya Taifa (Taifa Stars).

Hata hivyo, Azam itabidi iwe makini na safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiyumba katika michezi yake ya hivi karibuni ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Safu ya ulinzi ya timu hiyo inaongozwa kipa, Mwadin Ally, beki wa kati na David Mwantika na Joaqins Atudo wakati mabeki wa pembeni wanacheza Himid Mao na Wazir Salum.
Nafasi hiyo ya ulinzi imekuwa ikifanya makosa mengi kutokana na mara nyingine kutoelewana na hivyo kuruhusu mabao ya kizembe.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate