MECHI
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Yanga
iliyochezwa jana (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 66,568,000 kutokana na watazamaji 11,864.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0
kwa wenyeji wao vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24, Kamati ya Ligi sh. 4,790,670.24, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,395,335.12, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 931,519.21 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 931,519.21.
No comments:
Post a Comment