BEKI kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, amesema kuwa kwa hivi
hafikirii na hana mpango wa kuihama klabu hiyo yenye maskani yake mitaa
ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.
Nyota huyo alijiunga na
klabu hiyo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea Simba na
kuiwezesha Yanga kutwaa Ubingwa wa Kombe la Kagame 2012.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Yondani alisema bado ni mchezaji halali mwenye
mkataba na Yanga, hivyo malengo yake hivi sasa ni kuhakikisha anaisaidia
timu hiyo katika kutwaa ubingwa wa ligi na kwenye mashindano mbalimbali
ya kimataifa na kitaifa.
Yondani alisema, anafurahi kuwepo kwenye timu bora na ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya kimataifa.
Yondani alisema, anafurahi kuwepo kwenye timu bora na ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya kimataifa.
“Kiukweli
hivi sasa sifikirii kuihama Yanga na hakuna mpango wowote wa kuondoka,
ninachoangalia ni jinsi gani nitaiwezesha timu yangu kuchukua ubingwa wa
ligi.
“Tofauti na ubingwa, pia ni katika mashindano ya kimataifa tutakayoshiriki hapo baadaye na kikubwa nataka kucheza kwa kujitoa kwa nguvu zote ili tushinde mechi inayofuata kwa ajili ya kujihakikishia ubingwa,” alisema Yondani.

No comments:
Post a Comment