Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini
kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia
ukiukwaji wa maadili.
FIFA
ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti
kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya
baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe
30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo
yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa
TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye
kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013
na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa
FIFA, Jerome Valcke.
Malinzi (katikati) akiwa kwenye kikao cha kamati ya rufaa ya Mtinginjola ambayo hata hivyo haikumtendea haki |
Michael Wambura akiwa kwenye kamati ya Rufaa ya Mtinginjola pamoja na mwanasheria wake |
Mtinginjola akiendesha kikao cha kamati ya rufaa |
Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF
alifunga safari kwenda Dodoma jana kukutana na Mheshimiwa Waziri na
Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
“Matarajio yetu sote yalikuwa kupokea
majina ya waliopitishwa ili tufanye uchaguzi. Kinyume chake tumepokea
maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa hili ni jambo la kheri kwa vile
siyo tu haki itatendeka bali pia itaonekana imetendeka.” alisema Tenga,
ambaye alishatangaza kuwa hatagombea tena urais baada ya kuliongoza
Shirikisho kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.Endelea kusoma zaidi...
“Lengo letu ni kuhakikisha maagizo hayo
yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe
iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili
tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe
23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya
wagombea walienguliwa katika hatua ya mwisho na Kamati ya Rufani ya
Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika barua FIFA kuomba iingilie kati.
Rais Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA
ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba
baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni
suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu
nchini.
Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1. Kuunda
vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo
ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake
yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3. Kuanza
upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua
milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika kutekeleza hayo, TFF inatakiwa
iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya
Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za maadili na Kanuni za Uchaguzi
kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati Mpya ya
Utendaji.
Katika maoni yake FIFA imeeleza kuwa
katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua au kupitisha
baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni
za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha
suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za shirikisho na ukosefu
wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao
walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika (kamati za maadili) kabla
ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa
akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni
ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais
Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya
TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa
lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment