Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Utawala na fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani, Mama Lily Munanka, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe.
Liberata Mulamula na Dk. Nicku Kyangu Mordi.
Meza
kuu katika picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la
The Way of The cross Gospel Ministries yaliyofikia mwisho siku ya
Jumapili Aug 11, 2013 College Park Maryland.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika kwenye kanisa hilo College Park Maryland na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka DMV na majimbo ya jirani. Maadhimisho haya yalianzia Ijumaa na Jana Jumapili Aug 11, 2013 ndiyo ilikua hitimisho lililoambatama sala, nyimbo za injili kutoka vikundi mbalimbali wakiwemo waimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania Upendo Kilahiro na Christina Shusho waliokuja maalum kwenye maadhimisho hayo.
Juu
na chini ni Mhe. Balozi Mulamula akiongea na Watanzania waliohudhuria
maadhimisho hayo ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel
Ministries yaliyofikia mwisho siku ya Jumapili Aug 11, 2013 College
Park, Maryland.
Wachungaji kutoka makanisa mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 5 katika picha ya pamoja.
Upendo
Kilahiro, mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania akipamba jukwaa
kwa nyimbo mbalimbali siku ya mwisho maadhimisho hayo siku ya Jumapili
Aug 11, 2013, College Park, Maryland.
Mwimbaji
wa nyimbo za injili toka Tanzania, Christina Shusho akiimba moja ya
nyimbo zake siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The
Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika Jumapili Aug 11, 2013,
College Park Maryland.
No comments:
Post a Comment