Kahama.
Watu 13 wamepoteza maisha papohapo akiwamo mtoto mchanga wa miezi saba, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori la mizigo lililokuwa limeharibika barabarani katika Kijiji cha Ngongwa, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Watu 13 wamepoteza maisha papohapo akiwamo mtoto mchanga wa miezi saba, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori la mizigo lililokuwa limeharibika barabarani katika Kijiji cha Ngongwa, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati gari aina ya Toyota Hiace lilipoligonga lori.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kihenya
Kihenya, alisema Hiace hiyo ilikuwa ikifanya safari zake kutoka mjini
Kahama kwenda mji mdogo wa Ushirombo, katika Wilaya ya Bukombe, mkoani
Geita.
Kihenya alisema watu 11 akiwamo dereva ambaye pia ni mmiliki wa gari hilo, Ezekiel Werema, walifariki dunia papohapo na wengine wawili walifariki dunia wakiwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu.
Alisema polisi wanahangaika kutafuta majina ya marehemu na majeruhi, ili ndugu na jamaa zao waweze kutaarifiwa.
Pia, Kihenya aliwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano walioonyeshwa kwa polisi baada ya ajali kutokea na kuongeza kuwa, hadi sasa baadhi ya watu tayari wamejitokeza Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutambua maiti.
Kamanda Kihenya alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, huku akitoa wito kwa madereva kuwa makini wanapoendesha magari hasa nyakati za usiku.
Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali
ya Wilaya ya Kahama, Dk Joseph Fwoma alithibitisha kupokea maiti 11
kutoka eneo la ajali na kwamba, majeruhi wawili walifariki dunia
wakipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Wakati huohuo, Bakari Kiango anaripoti kuwa, polisi Kanda katika Maalum ya Dar es Salaam, wanawashikilia watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kwa tuhuma za kufanya uhalifu wakitumia sare za JWTZ na JKT.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana katika maeneo ya Temeke.
Alisema kukamatwa kwao kulikuja baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao kupanga kufanya uhalifu. Hilo ni tukio la nne kutokea ndani ya Agosti mwaka huu.
“Tutakomesha tabia hii ya watu kutumia sare hizi kwani imekuwa ikiwachanganya wananchi ambao wengi wao wakiwaona watuhumiwa hawa wanajua ni askari wa ukweli kumbe ni wahalifu,” alisema Kova.
Alisema walipopekuliwa watuhumiwa walikutwa na bunduki moja aina
ya Shortgun ikiwa imekatwa kitako ,maganda matano ya risasi za SMG na
bastola moja aina ya Browing ikiwa na risasi tano.
Hali kadhalika mkasi wa kukatia vyuma, kitambulisho cha JWTZz na sare mbili za Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate.
No comments:
Post a Comment