EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, September 4, 2013

Bale, Ozil, Fellaini watikisa barani Ulaya

London, England.
Masikio na macho ya mashabiki wa soka usiku wa kuamkia leo yalishudia timu mbalimbali za barani Ulaya zikikamilisha usajili wa nyota tofauti katika siku hiyo ya mwisho.
Mashabiki wa Arsenal na Manchester United walikuwa wakifuatilia kwa karibu uhamisho wa Mesut Ozil na Marouane Fellaini.

Taarifa iliyokuwa imetawala hadi tunakwenda mtamboni ni kiungo wa Real Madrid, Mesut Ozil kufanyiwa uchunguzi wa afya akiwa Ujerumani ili kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal baada ya kufikia makubaliano binafsi.Gunners walikubali kulipa euro 47 milioni kwa Real Madrid kufanikisha usajili wa kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani.


Kocha Arsene Wenger pia alikuwa akiendeleza jitihada zake za kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea, Demba Ba pamoja winga Angel Di Maria wa Real kwa gharama ya euro 30 milioni.


Kwa kipindi cha msimu wa likizo na usajili wa wachezaji, Arsenal imeshindwa kuwasajili wachezaji wa kiwango anachokitaka Arsene Wenger kama mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez na Gonzalo Higuain, mchezaji mwingine wa Real Madrid.


Lakini kwa sasa yumkini Ozil anaelekea Uuwanja wa Emirates kufuatia usajili wa Gareth Bale kwa kitita kikubwa cha pauni milioni 85.3.


Kabla ya kujiunga na Real Ozil alikuwa akichezea klabu ya Werder Bremen alikosajiliwa na Real kwa takribani pauni 12.4 milioni na kuichezea Real mara 155.

Pia, Manchester United walikuwa tayari kulipa pauni 30.5 milioni kwa ajili ya kiungo wa Athletic Bilbao, Ander Herrera, kwa mujibu wa Sky Sports.


Manchester United pia walikubali kutoa pauni 24 milioni kwa ajili ya kiungo wa Everton, Marouane Fellaini.


Hadi jana mchana Liverpool ilikuwa klabu ya England iliyofanya usajili mkubwa zaidi katika siku ya mwisho ya usajili.


Kocha Brendan Rodgers ameongeza wachezaji watatu Anfield, beki Mamadou Sakho, Victor Moses akitokea Chelsea kwa mkopo na beki wa kati Tiago Ilori kutoka Sporting Lisbon.

Wakati huohuo; Barcelona bado inatafuta beki wa kati, ambapo kocha Tata Martino anaendelea kujaribu kumshawishi beki wa Chelsea, David Luiz kwa gharama ya euro 25 milioni.


Hata hivyo Chelsea wenyewe wanataka Euro 40 milioni ili kumwachia Luiz.

Mbali ya Mbrazil huyo nyota mwingine wa Chelsea, Juan Mata aliivutia PSG waliokuwa tayari kutoa fedha.

Uhamisho
England
Tiago Ilori (Sporting Lisbon – Liverpool)

Mamadou Sakho (PSG – Liverpool)

Victor Moses (Chelsea - Liverpool)

Morgan Amalfitano (Marseille – West Brom)

Marko Arnautovic (Werder Bremen – Stoke)

Jack Hunt (Huddersfield - Crystal Palace)

Massimo Luongo (Tottenham - Swindon)

Francisco Junior (Everton - Vitesse Arnhem)


Abdul Razak (Manchester City - Anzhi Makachkala)


Harry Bunn (Manchester City - Sheffield United)


Italia

Kaka (Real Madrid - AC Milan)

Luca Marrone (Juventus – Sassuolo)


Hispania

Denis Cheryshev (Real Madrid - Sevilla)

Lisandro Lopez (Benfica – Getafe)


Ufaransa

Emmanuel Mayuka (Southampton - Sochaux)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate