STAA wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa
hawezi kurudia matapishi yake kwa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake,
Joseph Rashau ‘Bwana Misosi’.
Akichonga na paparazi wetu muda
mchache baada ya wadau kibao kumtaka mwanadada huyo arudiane na mpenzi
wake huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Amanda alisema tayari
ameshapenda kwingine hivyo hapendi kumzungumzia mtu aliyeachana naye pia
hana tabia ya kurudia matapishi yake.
“Siwezi kurudiana na Misosi
kwani nikishaachana na mtu basi ninamtoa moyoni mpaka mdomoni nikiwa na
maana sina muda wa kukaa na kumzungumzia ndiyo maana hata wadau
waliokuwa wakinitaka nirudiane naye sijawajibu chochote,”alisema Amanda.
CHANZO NI RISASI JUMAMOSI
No comments:
Post a Comment