Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi
halisia cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu
nchini Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema A. Sepetu, amepatwa na msiba
mkubwa.
Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.
Taarifa ambazo bongomovies imezipata zinapasha kwamba Mzee
Sepetu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na
kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia
akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini Dar-es-salaam. Mipango ya
mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini
Dar.
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya
Mwalimu Julius Kambarag Nyerere. Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini
Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa
Zanzibar, Dr Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment