KOCHA Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts, anatarajiwa kutua nchini Jumapili ijayo, wakati
huohuo ataanza mkakati wa kusaini mkataba mpya na timu hiyo.
Yanga inatarajiwa kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara hivi karibuni baada ya kumaliza ule wa kwanza ikiwa kileleni, lakini pia timu hiyo itakuwa inatumia nafasi hiyo kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo alimaliza mkataba wa kuitumikia Yanga kuanzia katikati ya mzunguko wa kwanza.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema wameshamalizana na kocha huyo, hivyo wanasubiri akitua tu nchini Novemba 24, ndiyo wamsainishe mkataba mpya.
“Brandts anatarajia kutua nchini Novemba 24, ambapo ndipo likizo yake itakuwa imefikia tamati kwa ajili ya kuja kukiandaa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi na michuano ya kimataifa.
“Mara tu atakapotua ndipo tutasainishana mkataba mpya, hadi sasa hatujajua tutamsainisha wa muda gani,” alisema Bin Kleb.

No comments:
Post a Comment