EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, November 23, 2013

KOPE BANDIA ZAMPOFUA MACHO MREMBO

AMA kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima.
Khadija Omar, mkazi wa Kigogo amepata pigo kufuatia kupofuka macho.
Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.
Akizungumza na paparazi wetu juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.
“Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.
“Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,”alisema Khadija.
Akaongeza: “Nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani,” aliongeza.                                                                                  Khadija Omar, mkazi wa Kigogo.
Khadija alisema kesho yake alikimbizwa Hospitali ya Amana, Dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa  Hospitali ya Macho ya CCBRT (Msasani, Dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo,” aliongeza Khadija kwa majonzi.
Alisema kule CCBRT alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.
Baada ya zoezi hilo kufanyika, Jumapili iliyopita Khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.
Jumatatu iliyopita Khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.
Daktari mmoja wa CCBRT ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: “Khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu’ iliyotumika.
Taarifa zaidi zinasema, Jane na Koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo Khadija  walikamatwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MGN/RB/13021/2013.
CREDIT: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate