EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, November 10, 2013

Lissu: CCM wana chuki na Warioba

MNADHIMU wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, jana alichafua hali ya hewa akisema kuwa CCM ina chuki na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Kwa mujibu wa Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Warioba na wenzake waliingiza mapendekezo ya serikali tatu kwenye rasimu, kinyume cha msimamo wa CCM.

Lissu aliibua tafrani hiyo bungeni jana wakati akichangia hoja ya kuunga mkono mapendekezo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, katika muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba akitaka mapendekezo ya serikali ya kuivunja Tume ya Katiba mara baada ya kukabidhi rasimu ya pili kwa Bunge Maalumu la Katiba yabadilishwe.

Badala yake, Mnyika alitaka tume hiyo iendelee na kazi hadi Bunge Maalumu la Katiba litakapomalizika ili kusaidia kutuoa ufafanuzi wa hoja zitakazojitokeza. 

Akichangia hoja hiyo baada ya wabunge kadhaa wa CCM kuwa wameipinga, Lissu alisema anajua kwanini hawataki.

“CCM wana chuki na tume ndiyo maana wanataka ivunjwe, isiwepo kabisa wakati wa Bunge Maalumu, sababu ni yule mzee Warioba kuingiza mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ambao hawautaki.   

“Kwa hiyo hawa wanataka wale wajumbe wasiwepo kabisa maana wameingiza mambo kinyume cha matarajio yao,” alisema Lissu na kuongeza kuwa CCM wamefikia hata hatua ya kupingana na mwenyekiti wao katika hilo.

Baada ya Lissu kuketi, Lukuvi alisimama kwa hamaki akiomba kutoa taarifa huku akijigamba kuwa lazima afichue siri ya jambo hilo ingawa hakutaka kufanya hivyo.

“Mh. Spika alichokisema Lissu ni uongo, CCM haijawahi kupendekeza jambo hilo. Naomba nitoe siri, maana mimi nilikuwa mwenyekiti wa vikao hivyo vya majadiliano kati ya rais na vyama,” alisema.

Huku wabunge wakimsikiliza kwa umakini, Waziri Lukuvi alisema pendekezo hilo lililetwa na CUF kwa maandishi chini ya uwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu wao (Bara), Julius Mtatiro.             

“Nasema siri hiyo ili mjue kuwa hilo ni wazo la CUF mshirika wa CHADEMA wala si la CCM,” alisema.

Wakati huohuo, Bunge lilikataa pendekezo jingine la Mnyika la kutaka idadi ya wajumbe wa tume wa kutoka kwenye makundi iongezeke kutoka 166 hadi 292, tofauti na pendekezo la serikali na kutoka 166 hadi 201.

Muswada huo ambao ulikuwa na mapendekezo matano ya serikali yaliyofikiwa baada ya majadiliano kati ya rais na vyama, ulipitishwa kwa pamoja na wabunge wote wakiuunga mkono.Chanzo Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate