MWENYEKITI wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Kata ya
Kahama Mjini wilayani hapa, Mkoa wa Shinyanga, Febronia Ikombe,
amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa kipigo na jamii ya wafugaji.
Mwenyekiti huyo anadaiwa kushambuliwa Jumanne iliyopita saa 5.00
asubuhi katika Kijiji cha Kanegele wilayani Masumbwe mkoa wa Geita baada
ya kundi la ng’ombe kuingia kwenye shamba lake la mpunga na kuharibu
mazao.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi nyumbani kwake baada ya
kutoka hospitali alikokuwa akitibiwa, Ikombe alisema siku ya tukio
alipokea taarifa kutoka kwa wakazi wa Kijiji cha Kanegele kwamba kuna
ng’ombe wameingia shambani kwake.
Ikombe alisema aliondoka na kwenda shambani akiongozona na watoto
wake watatu na dereva wake. Walipofika walikuta ni kweli ng’ombe hao
wakiwa shambani. Alisema kutokana na hali hiyo aliwafuata wachungaji wa
mifugo hiyo na kuwahoji kwa nini wameingiza mifugo shambani mwake.
Alisema hakupewa jibu, badaka yake mmoja wa wachungaji aliyejulikana kwa jina moja la Mwanasabuni alipiga mayowe hali iliyomshangaza Ikombe.
Alisema hakupewa jibu, badaka yake mmoja wa wachungaji aliyejulikana kwa jina moja la Mwanasabuni alipiga mayowe hali iliyomshangaza Ikombe.
“Mara niliona kundi la wanakijiji wakija shambani hapo wakiwa na
silaha za jadi, fimbo, mapanga na marungu, nilishtuka sana, nikamuuliza
Mwanasabuni kwa nini amepiga mayowe, hakunijibu,” alisema.
Alidai wananchi hao baada ya kufika walimshambulia kwa kuwapiga yeye na watoto wake wakitumia fimbo ambapo waliwajeruhi.
“Nimepasuka sehemu ya kushoto karibu na jicho, nilizinduka nikiwa
hospitalini ambako nilishonwa nyuzi sita. Mtu aliyenipiga namkumbuka ni
mgeni wa mwana kijiji cha Kanegele. Kwa kweli imenisikitisha sana,”
alisema mwenyekiti huyo.Credit GPL
No comments:
Post a Comment