Ndugu
zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na
niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi
kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata
habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.
Ndugu
waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie
kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa
gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu
ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na
kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana
wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa
kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila
uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.
Nadiriki
kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri
kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na
kuchaguliwa na watanzania.
Pia
itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama
ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za
kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya
chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali
cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na
juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru
wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya
chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha
nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na
kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo
limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi
tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere
ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.
Ndugu
zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana
wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha
kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga
chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama
ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na
kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa
najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha
mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa
chama kiko wapi?
Ukweli
ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani
kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais
2015 bila mafanikio.
Naomba
niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia
pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa
vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi
iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.
Kinachonisikitisha
zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni
pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA
na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.
Ninaomba
juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni
kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na
kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa
kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni
haya mpaka vijana ndio waone?
Kwa
hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri
-secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul
makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya
aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana
na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka
kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi
ya-wengine kupoteza mwelekeo.
Sisi
tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja
aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na
uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio
vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na
serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na
wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi
pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa
maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Mfano
hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana
kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala
havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.
Mwisho
Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu
makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi
kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment