
MAMBO 
yamekucha kwa kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya 
klabu tajiri ya TP Mazembe ya Lubumbashi, DR Congo kuonyesha wazi kuwa 
inamtaka.
TP Mazembe tayari imetuma mtu ambaye amekuja nchini kwa ajili ya 
kumshuhudia Messi akiichezea Simba na ameeleza nia ya klabu hiyo.
Shushu huyo wa usajili wa TP Mazembe alikuwa uwanjani wakati Simba 
ikicheza na Rhino ya Tabora kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili 
na kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Messi.
 
Habari za uhakika 
zimeeleza mara baada ya mtu huyo kumshuhudia Messi akifunga bao na pia 
kukosa penalti amewaeleza viongozi wa Simba kutokana na nia ya klabu 
hiyo maarufu barani Afrika.
“Jambo hili bado ni siri kubwa, lakini TP Mazembe walimtuma mtu wao, 
huyo ndiye alitumwa mara ya kwanza kuifanyia umafia Simba kabla ya TP 
Mazembe kuja hapa kucheza.
“Alipokuja akamuona (Mbwana) Samatta na kuwaambia kuna mchezaji 
hatari, ndiyo maana uongozi wote wa juu wa TP Mazembe ukaja kuja 
kushuhudia mechi hiyo na kweli Samatta akafanya vizuri.
“Kutokana na hali hiyo huyo jamaa anaaminiwa sana, akirudi na kusema Messi yuko safi, basi jamaa watakuja kufanya rasmi mazungumzo na Simba,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Kutokana na hali hiyo huyo jamaa anaaminiwa sana, akirudi na kusema Messi yuko safi, basi jamaa watakuja kufanya rasmi mazungumzo na Simba,” kilieleza chanzo cha uhakika.
TP Mazembe sasa inamlipa Samatta kitita cha dola 10,000 (Sh milioni 
16.5), kwa mwezi. Kama itafanikiwa kumpata Messi, basi huenda akachota 
kuanzia dola 3,000 hadi 5,000, kwa mwezi.
Messi amekuwa gumzo kuanzia mwanzo wa msimu huu kutokana na kiwango chake kupanda kwa kasi kubwa.
Messi amekuwa gumzo kuanzia mwanzo wa msimu huu kutokana na kiwango chake kupanda kwa kasi kubwa.
 
 
 
 
 
 
 

 
No comments:
Post a Comment