Mkuu
wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya,kikao kilichofanyika
mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi
wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele
ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi
wa wilaya mwishoni mwa wiki.
WANAFUNZI 1725 WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO
JUMLA
ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza
katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa
kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza katika kikao cha
Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango alisema wanafunzi wasioripoti kati
ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937 sawa na asilimia 56.1
Muwango alisema wanafunzi waliochaguliwa
kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni wanafunzi 3101 wavulana 1442,
wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na wasichana 10 wamechaguliwa
katika shule za bweni.
Alisema wanafunzi waliopangwa kwenda katika
shule za ufundi walikuwa wavulana 6 na hakuna msichana aliyechaguliwa
na wanafunzi 3074 walipangwa katika shule za serikali katika halmashauri
ya wilaya ya Kilolo.
Aliongeza kuwa wanafunzi walioripoti hadi
Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi 1349 wakiwemo wavulana 638 na
wasichana 711 sawa na asilimia 43.
Muwango alizitaja shule ambazo zina
asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni shule ya
Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi (19.3%),Udekwa (21%) na
Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi walioripoti.
Aliwataka walimu wa wakuu shule za
sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014
waliojiunga katika shule zao ili halmashauri iweze kujua na kujiridhisha
kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa taarifa kwa wanafunzi
wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata takwimu sahihi.
Alisema kuwa halmashauri imeandaa mikakati
kwa wanafunzi wasioripoti kwa kuwaandikia barua waratibu wote
kuwafatilia wanafunzi hao na kuwahimiza kuhudhuria katika shule
walizopangiwa.
Kwa upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita
amewataka watendaji wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila
kujali suala la ada na sare za shule.
Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.
Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.
“Haki ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana
na tusiache wazazi wanaowaficha watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao
kwa kuwaficha kuna kitu nataka kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni
kumwongezea thamani mtoto na mzazi mwenye katika maisha yetu ya kila
siku hivyo nawsisitiza sana watendaji wabaneni sana wazazi wote
wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule” alisema Guninita.
No comments:
Post a Comment