Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans
leo imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa
chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.
Young Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu
kufuatia kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na leo rasmi imeanza
mazoezi asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma
Pondamali.
Mkwasa alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji
wote waliofika mazoezini siku ya leo, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya
na kuzingatia mafunzo yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa
kiwango cha hali ya juu.
Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwafua
vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias
Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu kwani anaamini wachezaji hao
watakua katika kiwango kizuri kutokana na uwezo wanaouonyesha katika
mazoezi anayaowapatia.
Kikosi cha Young Africans kesho kitaendelea
na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.
Aidha
washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini
Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini
mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa
pili.
No comments:
Post a Comment