EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 11, 2014

MELI ILIYONASWA NA ‘UNGA’

Stori:  Waandishi Wetu
WIKI iliyopita Jeshi la Polisi Kikosi Kazi cha Wanamaji Tanzania, walikamata shehena ya madawa ya kulevya ‘unga’ wenye thamani ya mabilioni ya shilingi zikiwa ndani ya meli.

Wairan wakipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Taarifa za uhakika zinadai kuwa meli hiyo ambayo ni mali ya Kampuni ya  Almansoor SA ya Iran ilikamatwa Jumanne iliyopita katikati ya bandari za  Zanzibar na Dar es Salaam.

Meli hiyo ilikamatwa baada ya askari waliokuwa doria kuilitilia shaka na  kufuatilia kwa karibu ili kujua ilikuwa imebeba nini.

Vyanzo vilivyokuwa katika eneo la tukio  vinasema kuwa meli hiyo ilikuwa na watu 12 na baada ya kupekuliwa ndipo walikuta kilo 201 za madawa ya kulevya aina ya heroine.

Wairan wakiwa kizimbani.
Watu waliokamatwa katika meli hiyo ni Mohamed Hassan (30), Abdul Nabii (30), Fahiz Muhamad (34) na  Rahi Baksh (30), wote raia wa Pakistani.
Wengine ni Abdulsamad Badreuse (47), Hazra Azat (60),
Nahimu Musa (25), Khalid Ally (35),  Kher Murad (38), Said Mohamed (34), Murad Gwaharam (38) na Ayub Hot (50) ambaye ni nahodha wa meli, wote raia wa Iran.

Meli hiyo ilikuwa na mtazamo wa kivuvi na lengo la wahusika ilikuwa wasishtukiwe kirahisi.
“Ilikuwa si rahisi kuigundua kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo lakini askari wetu wana akili sana na ndiyo maana meli ile ilihisiwa mara moja,” alisema mtoa habari mmoja kutoka jeshi la polisi.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji Tanzania, ACP Mboje Kanga alisema ilikuwa ni kazi kubwa kuibaini meli hiyo ilikuwa imebeba nini lakini kwa kutumia mbinu za kiintelijensia waliweza kuitilia shaka na kuipeleka bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Uwazi, unga huo ulikuwa utue katika maeneo ya Ilala jijini Dar ambapo baadaye ungesambazwa kila kona ya nchi ya Tanzania.
“Ndugu waandishi, Ilala kuna maeneo ambayo ni maarufu sana kwa biashara kama hiyo, ule unga ulikuwa upelekwe Ilala halafu upelekwe nchi nzima,” kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa akizungumza na gazeti hili kuhusu madawa hayo, alisema kama yangefanikiwa kutua Dar na kusambazwa nchini watu milioni 3 mpaka 4 wangetumia, hasa vijana.

Kamanda Nzowa alisema meli hiyo ilitiliwa shaka  kutokana  na kutokuwa na utambulisho wa nchi husika, yaani bendera kama  meli zingine.
Akasema baada ya upekuzi waligundua  zaidi ya kilo 201 za heroin zenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 9.

“Mpaka sasa upelelezi unaendelea ili kubaini mwenyeji wao ambaye angewapokea Dar es Salaam ni nani maana kwa vyovyote yupo, tukimbaini amekwisha,” alisema Nzowa.
Waandishi: Haruni Sanchawa, Issa Mnally, Makongoro Oging’ na Richard Bukos.
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate