EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, March 28, 2014

Tambwe atangaza kuondoka Simba

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.
STRAIKA wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe huenda akavunja mkataba wake na klabu hiyo na kuondoka zake mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, ikiwa timu hiyo haitapata nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa.

Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe (kushoto) wakishangilia moja ya  bao katika Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tambwe ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19, amesema kuwa matarajio yake wakati anajiunga na klabu hiyo yalikuwa ni kuiona ikishiriki mashindano ya kimataifa, hivyo kukosa kushiriki michuano hiyo kutamtibulia mipango yake na ametamka wazi anafikiria kuondoka klabuni hapo.
Simba ipo katika nafasi ya nne na haina matumaini ya kushika nafasi ya kwanza wala ya pili kwa kuwa imesaliwa na michezo minne, ambapo imezidiwa pointi 10 na Yanga inayoshika nafasi ya pili.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe, raia wa Burundi alisema hatma yake ya kuendelea kubakia Simba itajulikana baada ya kumalizika kwa ligi ya msimu huu ambayo ipo katika hatua za lala salama.
Alisema anaweza kuondoka au asiondoke Simba lakini alisisitiza kuwa kila kitu kitajulikana baada ya Aprili 19 ambapo ligi itakuwa inafikia tamati.

“Wakati najiunga Simba, matarajio yangu yalikuwa ni kushiriki mashindano ya kimataifa, lakini ndoto hizo zinaonekana kugonga mwamba kutokana kwa kuwa hivi sasa timu yetu ipo kwenye nafasi mbaya ambayo haitupi kabisa matumaini ya kumaliza ligi tukiwa kwenye nafasi mbili za juu ambazo kwa sasa zinashikiliwa na Azam na Yanga.

“Kusema kweli hali hiyo inasikitisha na inaniumiza sana kwani natamani kushiriki mashindano ya kimataifa kama walivyo wachezaji wote wanaotaka mafanikio katika mchezo wa soka.
“Hata hivyo kwa sasa siwezi kuzungumza lolote kama nitaendelea kubakia Simba au la ila hilo litajulikana baadaye baada ya kumalizika kwa ligi kuu, lakini nafikiri juu ya hilo,” alisema Tambwe.
Simba ina pointi 36 nyuma ya Mbeya City yenye pointi 42, Yanga yenye ponti 46 na Azam inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 50.

Wakati huohuo, Tambwe amesema kama atapata nafasi ya kucheza kwenye mechi dhidi ya Azam katika ligi kuu keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, atapambana ili kuhakikisha Azam inafungika.
“Azam ni timu tu kama timu nyingine, naiheshimu kutokana na ubora wake, tutahakikisha tunaivunja rekodi yao ya kutofungwa msimu huu,” alisema Tambwe.
CHANZO CHAMPIONI IJUMAA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate