WANANCHI wa vijiji kadhaa vilivyomo katika Jimbo la Chalinze, ambalo Aprili 6, mwaka huu litafanya uchaguzi mdogo wa Ubunge, wamempa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Ijumaa katika vijiji saba vya jimbo hilo, wengi wa waliohojiwa kuhusu mshindi wa nafasi hiyo, walisema Ridhiwani anashika namba moja kwa vile ni mtu anayejua vizuri maisha ya watu wa Chalinze.
Walisema kitu kingine kinachofanya apewe nafasi ya kwanza, ni ukweli kwamba ni mtu mwenye ushawishi kwa watu wa makundi mbalimbali ambao anaweza kuwatumia kusaidia kutatua matatizo ya jimbo hilo ambalo aliyekuwa mbunge wake, Said Bwanamdogo alifariki mapema mwaka huu.
Wagombea wanaotarajiwa kuchuana katika uchaguzi huo mbali na Ridhiwani ni Mathayo Torongey (Chadema), Phabian Skauki (CUF), Vuniru Hussein (NRA) na Ramadhan Mgaya (ASP).
No comments:
Post a Comment