Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa
Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la
mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA
inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya
Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri
ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello
Bendera (kulia).
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo
mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto). Pembeni
ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,
Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu
(kushoto).
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole,
Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau
wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo
la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA
inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji
Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
Afisa
Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) –
Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa uzoefu wake katika moja ya Wilaya ya
Ilamba, Singida jinsi wananchi wanavyofaidika na TIKA.
Viongozi
wa Dini wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii
Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni
kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi
wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa
Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo
ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi
wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa
Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo
ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi
wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa
Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo
ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Mkuu Manundu, Korogwe Mzee Daffa Daffa.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akisalimia na viongozi wa dini wa
Halmashauri ya Mji Korogwe mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa
siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA)
ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza
jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Waheshimiwa
Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmshauri ya Mji Korogwe wakiwa katika
mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa
Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na
kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
NHIF
11: Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF)- Dar es Salaam, Genoveva Vicent akitoa majumuisho jinsi Mfumo wa
Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) unavyoweza kuwasaidia
wananchi.
Mchungaji
Joseph Mhina wa Kanisa la Anglikana Manundu, Korogwe akitoa shukrani
kwa wananchi waliofika katika mkutano huo wa wadau.
Timu
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dar es Salaam
na Tanga waliokuwa wakiratibu mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
na Mkuu wa Mkoa na Wilaya. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason
Blog.
---
MAAZIMIO YA KIKAO CHA WADAU WA TIKA KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE:-
1.
Washiriki wote wa kikao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga
wamekubaliana kwa kauli moja kukatwa Tshs.10,000 za posho zao kama
mchango wa TIKA ili kusaidia wazee na wenye mahitaji maalumu.
2. Kila mshiriki awe mwalimu na mhamasishaji kwa wale wote ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kikao hiki cha wadau wa TIKA
3.
Mfuko wa TIKA ni mali ya wana Korogwe hivyo kila mwananchi mwenye uwezo
na mfanyakazi achangie kiwango cha Tshs.10,000 kama mchango wa TIKA kwa
mwaka kwa mtu mmoja.
4. Watendaji wa Mitaa,Kata na halmashauri wawe karibu na wenyeviti wa mitaa katika kuhamasisha jamii kujiunga na TIKA.
5.
Kuhamasisha wanakorogwe walio nje ya Korogwe kuchangia Mfuko wa TIKA
kwa kiwango kilichowekwa ili kuuboresha mfuko na kusaidiwa wenye
mahitaji muhimu na wazee.
6. Wana Korogwe wenye uwezo zaidi kiuchumi waliopo Korogwe waombwe kuchangia mfuko huu ili kuuboresha.
7.
Kuhamasisha makundi maalumu kujiunga na TIKA mfano walemavu,na
wawakilishi wao waliohudhuria semina hii wakawe mfano kwa kujiunga na
TIKA na kuhamasisha wenzao.
8.
Watendaji wa Kata na Mitaa/Vijiji waitishe mikutano ya hadhara kwa
ajili ya uhamasishaji na washarikiane na washiriki waliopata
mafunzo/semina hii.
9. Viongozi wa dini watatumia vikao vya kidini kwa ngazi zote kitaka kuhamasisha jamii na waumini (misikitini na makanisani)
No comments:
Post a Comment