 Stori: Mwandishi Wetu
Stori: Mwandishi WetuMambo bado mabaya! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza, Risasi Jumatano linakuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, 
wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere 
‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, 
baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve 
kulifanyia kazi tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili 
wawakalishe chini.
“Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama
 hao kugombana, hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni 
kipindi cha kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala 
ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa kutaja majina ya wabunge 
hao na kutaka aulizwe Steve.
Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, 
ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu
 kati ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi 
wanatamani kuwa kama wao.
Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni  Idd Azan ambaye 
alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha 
mastaa hao.
CHANZO:GPL 
 
 
 
 
 
 
 



 
No comments:
Post a Comment