Stori: Waandishi wetu
KABAANG! Dokta mmoja aliyefahamika kwa jina la
Herman amenaswa katika dispensari moja iliyopo Buguruni Kwamnyamani
jijini Dar akijiandaa kumtoa mimba mwanafunzi.
Awali, kikosi kazi cha kufichua maovu cha OFM,
kilipewa malalamiko juu ya dispensari hiyo kuwa ni kinara wa mchezo huo
mchafu wa kuwatoa mimba mabinti wadogo hususan wanafunzi wa shule za
msingi.
Siku aliyonaswa, ilikuwa majira ya jioni ambapo kaka wa
mwanafunzi (jina tunalihifadhi) aliandaa mtego wa kumnasa daktari huyo
baada ya kupata taarifa kutoka kwa rafiki wa mdogo wake kuhusu mchezo
huo mchafu anaoufanya daktari huyo.
Kaka huyo aliwapigia simu makamanda wa OFM ambapo walitia timu
sambamba na polisi kwenda kuweka ‘kambi’ katika dispensari hiyo
kuhakikisha tukio zima linakuwa ‘recorded’.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari hiyo na kubana sehemu
kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku makamanda wa OFM
wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya eneo hilo.
Majira ya saa tisa, mwanafunzi huyo alifika hapo akiwa ameongozana na
kijana mmoja aliyesetiwa kuwa mpenzi wa mwanafunzi huyo na kuongea jambo
(kumpa fedha) na daktari akiingia chumbani akiongozana na mwanafunzi
huyo huko akiwa na vifaa maalum vya kutolea mimba.
Nesi,dokta chini ya ulinzi.
Baada ya kusubiri kwa dakika tano, kaka wa mwanafunzi huyo na
makamanda wa OFM waliingia katika chumba hicho na kumkuta daktari huyo
akiwa katika pilipilika za kumtoa mimba mwanafunzi huyo ambaye alikuwa
amelala chali.
OFM ilifanikiwa kunasa meseji mbalimbali za daktari
huyo zilizokuwa zikielekeza namna ya kufanikisha zoezi hilo la utoaji
mimba.
Majirani ambao walishuudia tukio hilo walipongeza sana OFM kwa
kumnasa daktari huyo kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo dispensarini
hapo.
”Jamani mmefanya vizuri sana kuja kukomesha mchezo huu hapa
tumelalamika sana lakini hatusikilizwi,” alisema mzee mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la mzee Hamisi.
Daktari huyo alipelekwa katika kituo kidogo cha polisi cha Buguruni
kisha kuchukuliwa maelezo ili hatua zaidi za kisheria dhidi ya daktari
huyo ziendelee.
Mpaka timu ya OFM inaondoka eneo la tukio hilo, walimuacha daktari
huyo akiwa anashikiliwa kituoni hapo na shauri lake likisomeka
MNY/RB/336/2014.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment