UHOLANZI
ni kama tayari imefuzu 16 Bora ya Kombe la Dunia kufuatia ushindi wa
3-2 dhidi ya Australia katika mchezo mgumu wa Kundi B Uwanja wa
Beira-Rio mjini Porto Alegre nchini Brazil.
Ushindi
huo, unaifanya timu ya Louis van Gaal itimize ponti sita baada ya mechi
mbili na kupaa kileleni mwa kundi hilo, ikiwa na mabao nane ya kufunga
na matatu ya kufungwa.
Kikosi
cha Australia kilikuwa: Ryan, McGowan, Wilkinson, Spiranovic, Davidson,
Leckie, Jedinak, McKay, Oar/Taggart dk77, Bresciano/Bozanic dk51 na
Cahill/Halloran dk69.
Uholanzi:
Cillessen, Martins Indi/Depay 45, Vlaar, De Vrij, Janmaat, De Jong,
Blind, De Guzman/Wijnaldum dk78, Sneijder, Van Persie/Lens dk87 na
Robben.
Mabao
ya Uholanzi yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 20, Robin Van Persie
dakika ya 58 na Memphis Depay dakika ya 68, wakati mabao ya Australia
yamefungwa na Tim Cahill dakika ya 21 na Mike Jedinak dakika ya 54 kwa
penalti.
No comments:
Post a Comment