Juzi, Nuhu Mziwanda alipost picha kwenye Instagram ikionesha Tattoo
aliyochora yenye jina la mpenzi wake Shilole ikiwa imeandikwa
‘ShiShiBaby’.
Sammisago.com ilipiga story na Nuh Mziwanda ili kuyakusanya majibu yote na kufahamu kiundani kuhusu uamuzi wake.
Mziwanda alieleza kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu katika kipindi
chote atakachokuwa duniani na kwamba haitafutika mpaka siku anaingia
kaburini.
Je, itakuwaje wakiachana (hatuombei iwe hivyo)? Nuh ameeleza kuwa yeye hajali kama wataachana au vipi kwa kuwa Shilole ni mtu muhimu sana kwake na amefanya kwa mapenzi yake.
“Nilimwambia labda wewe ndio utakaekuja kunizin
gua lakini mimi hata
siku moja sitakuzingua. Hata kama tukiachana, mimi nimeamua hivyo na
nimefanya kwa mapenzi yangu kwa sababu nampenda sana na ni mtu muhimu
sana kwangu.”
Kwa upande wa Shilole, alipost picha hiyo kwenye Instagram na
kuandika ujumbe wa kumshukurua mpenzi wake. “Thanx my lv 4 dis!
Umeonesha lv ya ukweli”
No comments:
Post a Comment