Baada ya Nuh Mziwanda kuamua kuchora tattoo isiyofutika ya jina la
malkia wake wa moyo Shilole aka ShiShi Baby, wengi walitoa mtazamo wao
kwa kuwa mapenzi ni…..!
Anyways, wahusika wakuu kwenye hii scene ya kweli ya mapenzi ni
Shilole na Nuh Mziwanda na tayari Nuh ameshaonesha mapenzi ya dhati kwa
mrembo Shilole.
Akizungumzia uamuzi wa mpenzi wake, Shilole amesema huo ni uamuzi mgumu sana aliouchukua na amefurahishwa sana na uamuzi huo.
“Hata sijui nisemeje…unajua kuchora kitu kwenye mwili ambacho sio cha
kwako ni ngumu sana. Kwa hiyo yeye uamuzi wake aliouchukua,
hakulazimishwa na mtu alifanya mwenyewe kwa mapenzi. Kwa hiyo aliamua
kwa kuwa analove na mimi na ninalove na yeye basi ndio maana akaamua
kufanya vile. Mimi kwangu ina maana kubwa sana sio siri ambayo
haielezeki.”
Shilole alizungumzia pia mpango wa kulipa wema wa Mziwanda kama nay eye atachora tattoo ya jina la Mziwanda au la!
“Hamna…siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu
na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye.
Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa
nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka
kutafuta ‘kick’ na nini…lakini Nu h kama Nuh ana upendo wa peke yake
kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu
akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”
No comments:
Post a Comment