LIPOISHIA WIKI ILIYOPITA Japokuwa
nimejitahidi sana kuisahau siku hii lakini moyo wangu umeshindwa kufanya
hivyo. Kila ninapotulia, iwe sebuleni au chumbani kwangu, picha ya siku
hiyo huwa inanijia kichwani mwangu. Tukio hilo limekuwa kubwa kwangu
huku likiendelea kujirudia kama mkanda wa filamu. SHUKA NAYO SASA…
Nilipenda
kwenda shule kusoma, na hii ilikuwa njia mojawapo ya kuepuka kufanya
kazi za nyumbani, hasa kuosha vyombo kitu nilichokuwa nikikichukia mno.
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini mama alijitahidi sana kuniweka katika mazingira ambayo mtoto wa kike anatakiwa kuwa.
Achukia kuosha vyombo
Kila siku alikuwa akinitaka nioshe vyombo,
hii ilikuwa kazi pekee niliyokuwa nikiichukia mno. Kila nilipokuwa
nikirudi nyumbani, mama alikuwa akinipa maziwa na kiporo cha jana,
nikimaliza kula, alikuwa akiniambia nioshe vyombo nilivyovitumia.
Nilikereka mno lakini sikuwa na jinsi, nilibaki nikilalamikalalamika
lakini mwisho wa siku niliosha vyombo mbele yake huku akionekana kuwa na
furaha.
AWA KIONGOZI WA KUIMBA
Ijulikane kwamba kuimba
ni kipaji nilichozaliwa nacho. Nakumbuka kipindi hicho mimi ndiye
nilikuwa kiongozi wa nyimbo mbalimbali tulizokuwa tukiimba shuleni.
Sauti yangu haikuwa nzuri, ilikuwa ni ya kukoroma sana lakini kila
nilipokuwa nikiimba walimu waliipenda na ilikuwa ni lazima ujue kwamba
‘huyo anayeimba ni Lusako’.
AANZA DARASA LA KWANZA
Baada ya kusoma shule ya
chekechea kwa miaka miwili, mwaka 1990 nilitakiwa kwenda kuanza darasa
la kwanza katika Shule ya Msingi Muungano ambayo haikuwa mbali kutoka
tulipokuwa tukiishi.
Kama kawaida yangu, siku hiyo niliamka asubuhi sana huku nikiwa na
hamu ya kuanza darasa la kwanza. Moyo wangu haukuweza kusahau, bado
niliendelea kukumbuka miaka miwili iliyopita ambapo nilishindwa
kulishika sikio langu la upande wa kushoto kwa kutumia mkono wangu wa
kulia kwa kuupitisha kichwani.
Kwanza kabla ya yote, hapohapo nyumbani, nikajaribu kulishika sikio langu, nikafanikiwa.
ACHEKELEA KUJIUNGA NA SHULE YA MSINGI
Naweza
kusema kwamba katika mwaka huo, siku hiyo ndiyo nilikuwa na furaha
kupita kawaida. Nilipenda sana shule, kila nilipokuwa nikiwaona
wanafunzi wakipita nyumbani huku wakiwa wamevalia sare zao za shule,
niliona wivu moyoni.
Leo hii na mimi nilitakiwa kwenda kuanza darasa la kwanza! Asubuhi ya
siku hiyo, mama akaniletea sketi na shati huku chini nikivalia soksi za
pundamilia.
Sikuwa na sare za shule hivyo siku hiyo nilivalia nguo
za nyumbani ila miguuni nilikuwa na soksi hizo za pundamilia. Baada ya
kutembea kwa umbali mdogo, nikaelekea shuleni huku nikiongozana na baba,
mzee Bukuku.
Watoto waliokuja kuanza shule walikuwa wengi na zoezi lilikuwa
lilelile la miaka yote, kushika sikio lako. Wapo walioshindwa ambao
walilia kama nilivyofanya miaka miwili iliyopita lakini pia walikuwepo
wale waliofaulu na kutakiwa kujiunga na shule hiyo kwa ajili ya kuanza
na elimu ya msingi huku nikiwa nimeandikishwa jina jingine na kuitwa
Bahati.
*** AANZA MASOMO
Niliipenda masomo, niliipenda shule kwa jinsi majengo yake yalivyokuwa.
Yalipendeza na kuvutia sana. Siku hiyohiyo ambayo baba alikuwa
amenipeleka shuleni hapo, tukaingizwa darasani na kupangwa, siku
iliyofuata, tukaanza masomo huku tukiwa watoto zaidi ya arobaini katika
darasa moja.
Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kama nilivyokuwa. Hakukuwa na
utulivu, kila wakati wanafunzi walikuwa wakipiga kelele, nadhani kwa
walimu au kwa watu waliokuwa katika mitaa yenye watoto wengi watakuwa
wanalitambua hili, jinsi watoto wanavyopiga kelele zenye kuleta kero.
AONGOZA KWA UTUNDU
Kati ya wanafunzi wote
waliokuwa darasani, mimi ndiye nilionekana kuwa mtundu. Kwanza sikutulia
sehemu moja, nilionekana kama mtu aliyekuwa akitafuta kitu fulani, muda
huu unaweza kuniona hapa na baadaye kuniona kule.
UTUNDU WAMPA UMONITA
Kutokana na utundu wangu wa
muda mfupi, hata mwalimu wa darasa hilo aitwaye Rugemilila alipoingia
darasani, akanichagua niwe ‘monita’ yaani kiongozi wa darasa lile.
Maisha ya nyumbani yaliendelea kuwa vilevile kwamba kila nilipokuwa
nikirudi na kula chakula, mama alinitaka nioshe vyombo. Bado mama
alinifundisha mambo mengi huku akitamani sana niwe kama wasichana
wengine, nadhani mbele ya maisha yangu aliyaona kwani kwa kile
alichokuwa akikitaka ndicho kimeweza kunisaidia sana kipindi hiki.
AKAMUA NG’OMBE MAZIWA
Kazi zote za nyumbani
ambazo alikuwa akizifanya mama, ilikuwa ni lazima na mimi nizifanye.
Siku ambayo sikuwa nikienda shule, ilikuwa ni lazima nipike japo chai na
kufanya usafi nyumbani hapo huku nikisaidiana naye.
Nyumbani kulikuwa na ng’ombe, kila siku, hata kabla ya kwenda shule
ilikuwa ni lazima niamke asubuhi sana, nikamue maziwa na kisha mtu
ambaye alikuwa akihusika kwa ajili ya kwenda kuwachunga akiwatoa zizini
na kwenda nao machungoni.
ACHUNGA NG’OMBE
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu
ya kila siku. Siku ambazo sikuwa nikielekea shuleni, pia nilikuwa
nikichukuliwa na kupelekwa machungoni. Nilichukia kazi nyingine lakini
hii ya kuwapeleka ng’ombe machungoni niliipenda kwa sababu ilinipa
nafasi ya kuondoka nyumbani hapo kwenda kuzurura na ng’ombe hao.
AUZA CHIPSI
Kutokana na utundu niliokuwa nao na
ujanja wa hapa na pale, mwalimu wangu wa darasa akanichagua niuze chipsi
zake. Wanafunzi wengi walikuwa wakiitamani kazi hii kwani walijua fika
kwamba mara unapouza na nyingine kubaki, walimu huwa na kawaida ya
kukupa mfuko mmoja ule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment