EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, June 21, 2014

VICKY KAMATA AFANYIWA SHEREHE

BAADA ya kimya kirefu tangu ndoa iliyopagwa kufungwa kati yake na Charles Pai kuyeyuka, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha vijana Mkoa wa Geita, Vicky Kamata ameibuka na kufunguka mambo mengi lakini kubwa ni kwamba, amefanyiwa sherehe.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha vijana Mkoa wa Geita, Vicky Kamata akiwa Bungeni.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, juzi Alhamisi kwa njia ya simu akiwa bungeni Dodoma, Vicky alisema watu wamezungumza mengi kuhusiana na ishu ya ndoa yake kuhairishwa lakini hakuna alisema ukweli.
“Watu wanaongea sana. Wamezungumza mengi lakini mimi ndiye mwenye ukweli. Nawashukuru sana wale ambao wamekuwa upande wangu katika kipindi kigumu nilichopitia.
“Ilifikia hatua baadhi ya wabunge wenzangu wanawake waliamua kunifanyia dinner party (hafla ya mlo wa usiku). Ilinifariji sana, wengine ni watu wazima, mama zangu walinipa moyo sana kwa yaliyotokea.
“Walikuwa wabunge wengi, nakumbuka hata mama zangu, Tibaijuka (Ana – Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi) na mama Kilango (Anne Malecela – Mbunge wa Same Mashariki) walikuwepo,” alisema na kuongeza:
Vicky Kamata akiwa na mchumba wake Bw. Charles Pai.
“Walinipa moyo, wakaniambia nitulie nifanye kazi. Kila kitu namwachia Mungu. Walinichangia mpaka fedha, kwa kweli nawashukuru sana kwa kampani yao, wote wanajijua, siwezi kuwataja wote.”
MADAI YA MUME WA MTU
“Kuna watu wanapakaza kuwa, eti mchumba wangu ni mume wa mtu ndiyo maana tukashindwa kufunga ndoa, siyo kweli. Nakiri kwamba aliwahi kuoa na aliachana na mke wake kisheria tangu mwaka 2012.
“Watu waache kuzungumzia mambo wasiyoyajua. Mimi ndiye ninayeujua ukweli, lakini najua wabaya wangu ndiyo wanaosambaza hayo maneno yasiyo na ukweli,” alisema Vicky.
AWACHANA WABAYA WAKE
“Ni vile watu hawaelewi, lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi ya wabunge wana uadui na mimi. Hao ndiyo wanaosambaza habari za uongo magazetini. Kuna mwanamke aliibuka, akasema mchumba wangu ni mume wake, haikuwa kweli.
Vicky Kamata akiwa na familia yake.
“Huyo dada alitumwa na hao wabaya wangu ili wanivurugie mambo yangu ya kisiasa tu. Hizo ni njama za wabunge wasionipenda, ni mchezo mchafu wa kisiasa. Mara nyingi nasema hiyo ni siasa majitaka.
“Kama nilivyokuambia, aliyekuwa mkewe waliachana tena kwa taratibu zote, siye aliyesema kuwa nafunga ndoa na mumewe. Yule dada ni mtu mzuri, ana moyo mzuri, hana makuu sema huyo aliyeharibu shughuli yangu alitengenezwa na wanasiasa wenzangu ili waniharibie na kunivuruga kiakili, nasema wameshindwa.”
PAI KUTOROKA NA MICHANGO
“Wamesema mengi, wamenichafua kwa mengi, hadi wamefikia hatua wakasema mchumba wangu ametoroka na michango kiasi cha milioni arobaini – si kweli.
“Mchumba wangu yupo hapa nchini na anaendelea na kazi zake kama kawaida. Lilikuwa zengwe tu lililotengenezwa na baadhi ya wabunge wapinzani wangu ili waniharibie.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate