EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, June 21, 2014

WAKATI MBASHA AKIWA HURU KWA DHAMANA, GWAJIMA APASUA JIPU!

Stori: Haruni Sanchawa na Richard Bukos
WAKATI mume wa mwimba Injili Bongo,  Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiachiwa huru kwa dhamana kufuatia kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima ameibuka na kunena mazito kuhusiana na sakata hilo, Risasi Jumamosi limesheheni mkobani.
Mbasha akiwa na Pingu.
Mbasha aliachiwa kwa dhamana juzi akitokea Gereza la Keko, Dar baada ya kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juni 17, mwaka huu na kusomewa mashitaka mawili ya ubakaji ambayo hata hivyo, aliyakana.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima.
ILIVYOKUWA KORTINI
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mheshimiwa Wilbeforce Luago siku hiyo ya Juni 17, alitoa hoja kwamba upande wa jamhuri hauna pingamizi hivyo dhamana ipo wazi.

Emmanuel Mbasha akielekea kizimbani.
Alisema mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, mfanyakazi wa serikali na wa kutoka katika taasisi inayotambulika sanjari na shilingi milioni 5 kila mmoja. Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo siku hiyo hadi hadi juzi alipotimiza, akaachiwa.
Mume wa mwimba Injili Bongo,  Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa chini ya ulinzi.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ambaye ni wakili wa serikali, Nassoro Katuga bila kuchelewa aliitaja kesi hiyo yenye namba CC/186/2004 ambapo rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa aitwaye Mwahimu Juma ndiyo waliofanikisha dhamana hiyo. Kesi yake itatajwa tena Julai 17, 2014.
Bw. Emmanuel Mbasha akiondoka baada ya kupewa dhamana.
GWAJIMA SASA
Akizungumza na paparazi wetu juzi wakati Mbasha akiwa nje kwa dhamana, Mchungaji Gwajima alieleza namna ambavyo sakata hilo limeitikisa Injili nchini Tanzania kutokana na kuibuka kwa madai mengi likiwemo suala la Flora kusemekana amehamia nyumbani kwake kitu ambacho alikipinga.
Gwajima alisema anasikitika sana kuona ndoa ya Flora na Emmanuel Mbasha inatikisika akizingatia Flora ni muumini wake hivyo moja kwa moja ugomvi wao unaonekana kutia dosari mwenendo mzima wa uinjilishaji katika jamii.
“Naumizwa sana na sakata hili lakini hivi karibuni niliamua kuwaita ndugu wa pande zote mbili (Flora na Mbasha) nikazungumza nao kwa kirefu na tukamaliza tofauti zote lakini tatizo likabaki lile la kisheria zaidi (mashitaka ya ubakaji kwa Emmanuel),” alisema Gwajima ambaye makao makuu ya kanisa lake yapo Kawe jijini Dar.
AANDAA TAMKO ZITO
Mchungaji Gwajima alisema kutokana na sakata hilo kugusa Injili, ameandaa tamko zito ambalo atalitoa rasmi atakaporudi safari yake ambayo hakueleza anakokwenda.
“Hatuwezi kukaa kimya juu ya hili, nasafiri lakini nikirudi tu nitatoa tamko rasmi kwa kuwaalika waandishi wa habari,” alisema.
IBADANI JUMAPILI
Katika hatua nyingine, ndani ya ibada ya kanisa hilo iliyofanyika Jumapili iliyopita, Mchungaji Gwajima alitumia dakika kama 15 katika mahubiri yake kutupa kile kilichodaiwa kuwa ni jiwe gizani ambapo wengi waliamini ni kuhusiana na sakata hilo.
“Mimi siyo kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga halafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana chizi? Tatizo la Watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee, lakini mimi siyo kama wao,” alisema.
Aliongeza: “Mimi kila mwaka naenda Japan na ninawa-lecture Wajapani ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini Watanzania hawashtuki na kuja kujifunza juu ya ufufuo wa wafu wengi wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi siyo kama wale.”
AMEFUNGUKIA SAKATA LA MBASHA?
Ingawa Mchungaji Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la Mbasha lakini maneno hayo yalitafsiriwa kwamba ni ya kujibu hoja zinazomhusisha yeye na tukio hilo.
Anaendelea:”Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani na nyingi za Ulaya na Marekani halafu mtu amekaa Magomeni miaka yote anatengeneza stori ya gazeti, unatarajia niijibu, mimi siyo kama wale nimetumwa na nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi kufa mpaka niimalize.”
Ndugu na jamaa wa Emmanuel Mbasha waliofika mahakamani.
AYAGEUKIA MAGAZETI
“Inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwatungia stori hizo za uongo lakini mimi siyo kama wale na mwezi huu wa nane ninaendelea na mkutano Iringa, waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na siyo kama wale.”
DONGO GIZANI?
Baadhi ya waumini waliokuwa katika ibada hiyo, walibaki njia panda na katika giza nene ingawa wengi waliamini alitupa vijembe katika sakata la Mbasha haswa alipokuwa akisema, ‘mimi siyo kama wale’.
ILIWAHI KUANDIKWA
Katika Gazeti la Uwazi, toleo la Juni 10, 2014  kulikuwa na habari ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa; Mbasha: Gwajima nianchie mke wangu.
Katika habari hiyo, Mbasha alishangazwa na kusikia habari kwamba, baada ya kutofautiana na mke wake na kutokea madai ya kumbaka shemeji yake, mkewe alihamia nyumbani kwa Gwajima kujisitiri lakini madai hayo, Gwajima aliyapinga vikali. Baadaye ilibainika kuwa, Flora anaishi hotelini Sinza, Dar.
ANGALIA GLOBAL TV ONLINE MUDA WOTE KWA HABARI MOTO MOTO; KUINGIA, BONYEZA BANNER HAPA CHINI:

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate