EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, June 16, 2014

WEMA, KAJALA BIFU UPYA!

ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu kuripotiwa kupatanishwa kwa mastaa wawili katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja, taarifa zisizo na shaka zilizotua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda zinaeleza kwamba upatanisho huo haukusaidia chochote na sasa bifu jipya limeibuka kati yao.
Wema Sepetu akipozi pembeni ya ndinga yake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kilichoomba hifadhi ya jina lake, zoezi la upatanishi kati ya mastaa hao lililofanyika kwenye msiba wa dairekta wa filamu za Kibongo, George Tyson, Mbezi Beach jijini Dar lilikuwa sawa na kazi bure.

“Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na nia ya dhati ya kumaliza tofauti zilizokuwepo, walikubali kupatana kwa sababu ya heshima ya waliokuwa wanawapatanisha lakini kiukweli ilikuwa ni sawa na danganya toto, bifu limelipuka upya,” kilisema chanzo hicho ambacho ni rafiki wa karibu wa mastaa hao wakubwa mjini.
TEAM WEMA, TEAM KAJALA WANOGESHA BIFU
Kwa mujibu wa sosi wetu, ukiachilia mbali kukosekana kwa utayari wa kupatanishwa kati ya wawili hao, pande mbili za mashabiki wao wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii waliojipachika majina ya Team Wema na Team Kajala, zimekuwa zikinogesha bifu hilo kwa kumwagia petroli kwenye moto, hali inayozidi kutibua mambo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
“Sikia nikwambie, kuna vitu vinafanyika katika mitandao ya kijamii hasa Instagram kuhusiana na hizi pande mbili halafu wahusika wakuu wanajifanya hawazijui, kuna Team Wema ambayo inamsapoti Wema na ile ya Kajala inayoitwa Team Kajala, wenyewe wanawajua fika ni akina nani wanaounda pande hizo ila ukiwauliza wanajifanya hawajui chochote.
“Wengine wananunuliwa mpaka simu za kisasa zenye uwezo wa kufungua mitandao ya kijamii ili wasambaze uzushi na uongo kuhusu upande pinzani, sasa timu hizo ziliposikia juu ya upatanisho huo, ziliwajia juu wahusika ambapo kila mmoja kwa upande wake alikanusha kupatana na mwenzake,” kilizidi kutiririka chanzo hicho.
Mastaa hao wawili wakiwa katika picha ya pamoja.
KAJALA HATAKI KABISA SULUHU
Chanzo chetu kiliendelea kufunguka kuwa Kajala hataki kabisa kusikia kuhusu mambo ya suluhu kwa sababu Team Wema imemdhalilisha sana mtandaoni kiasi cha kumpa wakati mgumu kujieleza mbele ya mwanaye, Paula ambaye inadaiwa naye aliyashuhudia matusi hayo ya nguoni.
“Yaani Kajala anasema labda Wema mwenyewe ndiyo aende kumuomba radhi kwa kashfa zilizokuwa zinatolewa na timu yake anaweza kumfikiria mara mbilimbili kuhusu suluhu na siyo kusuluhishwa juujuu tu kama ilivyotokea,” alizidi kutiririka sosi wetu na kuongeza:
“We si unaona mara ngapi Wema na Kajala wanakutana sehemu na wewe mwenyewe kama mwandishi unashuhudia, umewahi kuwaona wakiwa pamoja au hata kusalimiana?”
MSIKIE KAJALA
Baada ya kusikia  kauli hizo kutoka kwa chanzo chetu, kama kawaida ya Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kutafuta mzani wa habari ambapo wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Kajala ambaye hakutaka kabisa kulizungumzia kwa kina suala hilo. Hebu msikie:
“Kiukweli mi naona hili tatizo letu linachangiwa na hizi timu ambazo zipo kwa ajili ya kuongeza matatizo. Nasikia eti baada ya siku ile mimi na Wema kupatanishwa, watu wa timu yake walimpigia kumuuliza, akakataa kuwa hajakubali kupatanishwa na mimi ili kuwafurahisha watu wake, sasa unategemea mimi nitasema nini? Nafikiri siyo rahisi mimi kukaa karibu na Wema kama zamani,” alisema Kajala.
WEMA NAYE
Kwa upande wa Wema yeye alishangaa habari hizo na kutoa dukuduku lake kwa kusema anachojua ni kwamba hana bifu na mtu yeyote, siyo Kajala tu bali mtu yeyote ambaye walikuwa na tofauti huko nyuma yeye hana bifu naye tena.
“Mi nadhani watu wanahitaji kuona picha ambayo tumepiga pamoja na Kajala ndiyo waamini kuwa tumemaliza bifu letu, unajua huu unaokuja ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na mimi ni mtoto wa Kiislam sasa nitafungaje Ramadhan huku nikiwa na bifu na mtu?” alisema Wema.
Kukinzana kwa maelezo ya wawili hao kunatosha kuonesha jinsi ambavyo suluhu ya awali haikuweza kumaliza bifu kati yao.
KUTOKA KWA MHARIRI
Wema na Kajala nyie ni wasanii wakubwa ambao jamii inawatazama kama kioo chao. Haipendezi kuendeleza malumbano yasiyo na msingi, huu si wakati wa kuwekeana visasi bali sameheaneni kutoka ndani ya mioyo yenu na mshirikiane kuisimamisha sanaa ya filamu za Kibongo.
CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate