EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, June 30, 2014

WEMA NA KAJALA WAMEPATANA

Stori:  WAANDISHI WETU
Hatimaye! Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa na kusababisha tafrani kubwa, Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ hatimaye wamekutana uso kwa uso (live) na kumaliza bifu lao saa chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Ijumaa Wikienda limesheheni.
Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ wakikata mauno.
NI KWENYE VUNJA JUNGU
Tukio hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa staa mwenzao wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Mwananyamala jijini Dar ambapo baadhi ya mastaa walikuwa wakivunja jungu katika sherehe ya kumpongeza rafiki yao almaarufu kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto wa kike hivi karibuni.
...Wema na Kajala katika pozi.
KWA MARA YA KWANZA TANGU WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa na butwaa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu wagombane. miezi kadhaa iliyopita.
WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama kumbikumbi wakila ujana kama zamani, kitendo kilichowafurahisha marafiki zao wengine waliofika nyumbani hapo wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja kwani tangu wapatanishwe hawakuwahi kukaa pamoja wala kula sahani moja kama walivyofanya siku hiyo.
...Wema na Kajala wakila sahani moja kwa furaha.
“Ukweli sisi tumefurahishwa na ukaribu wa hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao kata, leo wameshirikiana kama zamani, wamezungumza, wamecheka na kukata mauno pamoja,” alisikika mmoja wa mastaa aliyehudhuria katika shughuli hiyo.

MAUNO MWANZO-MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno mwanzo-mwisho yaliyoongozwa na wapiga ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja aliinuka na kuonesha ustadi wake wa kukata mauno.
Aunt Ezekiel na Vanita wakikata nyonga.
HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani baada ya Kibao Kata, mastaa hao walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na madj maalum wa Pro24djs huku MC akiwa ni Maimartha  Jesse.
WEMA, KAJALA, AUNT WAPAGAWISHA
Katika shughuli hiyo, Wema, Kajala na Aunt walipagawishwa na wimbo wa mpya wa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wa Mdogomdogo ambapo waliingia kati na kuachia mauno hadharani.
...Aunt Ezekiel na mashosti zake wakizidi kuonyesha machejo.
Kuna wakati Kajala na Wema waliachiwa nafasi ambapo walitoana jasho kwa kukata mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo utadhani walikuwa wamefanya ‘riheso’.
ASANTE DJ
Baada ya kuserebuka kwa muda mrefu hadi wakatoka jasho, wawili hao walisikika wakisema kuwa Dj alikuwa amewakuna mno kwani kila muziki aliokuwa akiwawekea alikuwa akiwalenga na kuwafanya wachangamke zaidi hadi shughuli ilipokwisha kila mtu akarudi kwake.
NENO LA WEMA
“Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega kwa bega ukizingatia ndiyo tunaingia kwenye mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti na Kajala,” alisema Wema.
NAYE KAJALA
“Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi sana,” alifunguka Kajala.
Mahasimu hao wawili wakiwa kwenye picha ya pamoja na mashosti wenzao.
TUMEFIKAJE HAPA
Miezi kadhaa Wema na Kajala waliingia kwenye gogoro kubwa na kusababisha kuibuka kwa pande mbili za Team Wema na Team Kajala zilizokuwa zinachochea ugomvi huku Kajala akitakiwa kurejesha zile Sh. Milioni 13 alizolipiwa na Wema asiende jela miaka 7.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Hongereni Wema na Kajala kwa kutambua umuhimu wa kuishi kwa amani na kumaliza tofauti zenu. Sasa ni muda wa kufanya kazi kwa bidii.
Imeandikwa na Gladness Mallya, Hamida Hassan na Musa Mateja.
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate