EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 1, 2014

DAKTARI, MGONJWA LIVE


AMA kweli majanga yakimkuta binadamu hayapigi hodi! Daktari wa meno aliyejulikana kwa jina la Dokta Ngariba (54), amejikuta ndani ya janga la tuhuma za ngono baada ya wapiga picha wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kunasa sakata lake na mwanamke aliyedai ni mgonjwa wa jino aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamida (20).
Dokta Ngariba akijitetea.

Tukio hilo la kushangaza lilijiri Juni 9, mwaka huu ndani ya Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kilichopo Kigamboni jijini Dar ambapo timbwili hilo lilitokea.
ILIKUWAJE?
Ilikuwa wakati OFM wakizunguka katika Jiji la Dar es Salaam kama ada kusaka matukio ndipo walipopita nje ya kituo hicho walisikia sekeseke kutokea kwenye chumba ambacho baadaye kilibainika na cha kung’olea meno.

UCHUNGUZI, UFUATILIAJI
Katika uchunguzi na ufuatiliaji wa OFM, mgonjwa huyo alisikika akidai kwa polisi waliofika kutuliza sakata kuwa, alijihimu kwenye kituo hicho kwa lengo la kung’oa jino lakini katika hali ambayo hakuitarajia daktari huyo alimtaka kimapenzi naye akajikuta akitumbukia.

....Akiandaa zana za kazi.
HEBU SIKIA HII
“Mimi nimekuja kung’oa jino, linaniuma leo sijui siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka kimapenzi. Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria,” alisema mwanamke huyo ambaye alikutwa ameshavua dera.

UTETEZI WA DAKTARI
Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha mgonjwa wake huyo atambe kiasi hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa, alimpokea mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha kung’olea meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha kumvua na yeye shati na baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.

.....Wakiwa chumba cha kung'olea jino
Akiendelea kuzungumza mbele ya Polisi wa Kituo cha Kigamboni waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha matibabu ya meno, daktari huyo alisema:
“Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua ni mgonjwa anataka tiba ya kung’olewa jino.
“Sasa nikiwa katika maandalizi ghafla nikamwona anavua nguo na kisha akanivaa mimi na kuanza kunivua shati. Nashangaa sana anaposema nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani.”

MASWALI MAGUMU
Baada ya maelezo ya Dokta Ngariba, OFM ilikuwa na maswali yake lakini haikupewa nafasi ya kuyauliza kwa vile walidandia ishu.

.....Wakielekea kituo cha polisi Kigambono.
Swali la kwanza; kama kweli Dokta Ngariba alivamiwa na kuvuliwa nguo na mgonjwa huyo, alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa watumishi wenzake?
Swali la pili; mpaka mgonjwa anajivua nguo zake kisha kumvua yeye shati na baadaye kuelekea kwenye fraizi ya suruali, yeye alikuwa anawaza nini akizingatia ni mgonjwa wa meno? 
Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:

“Taarifa hizo nazisikia kwako, niko safarini, nitafuatilia. Kama ni kweli hatua zinachukuliwa kwa waajiri wake ambapo najua kwa kosa kama hilo ni kupoteza kazi.”
Stori: Chande Abdallah, Issa Mnally na Richard Bukos

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate