Hatimaye mshamabuliaji Geilson Santos Santana
"Jaja" raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016)
kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali
ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika mwakani.
Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema
usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa
baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia
ni raia wa Brazil.
"Kazi yetu uongozi ni
kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa
mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili
yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.
Jaja
ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa
Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans
alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu
katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi
wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans
kwa ajili ya michuano mbalimbali.
No comments:
Post a Comment