Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendi ya Vijana Jazz.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa
zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika
bendi ya umoja wa vijana, Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa
kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha,
Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013
akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemed
Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu
mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka
marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti
zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz
imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake
yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga
Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.
Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa
ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye
mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa
(Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji
kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.
Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao
waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah
Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki
wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya
mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa
Fahad. Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi
lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na
kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili
halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea
vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo
na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai
chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed
Maneti upo na siwezi kuuepuka... lakini kubwa watu wananipima kutokana
na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".
No comments:
Post a Comment