STAA aliyeitendea haki sinema ya Kigodoro, Riyama Ally amesema licha ya kuwa ana mchumba lakini hayupo tayari kuolewa kwa sasa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Riyama alisema hahitaji kuolewa kwa
sasa kutokana na kushuhudia ndoa nyingi za mastaa zikivunjika, hivyo
anahitaji muda mwingi wa kufikiria juu ya mtu wa kuingia naye kwenye
ndoa.
“Nitaolewa baada ya moyo wangu kuwa tayari kwani ndoa si jambo la kukurupuka, lazima uwe na mtu sahihi,” alisema Riyama.
No comments:
Post a Comment