Watumishi
wa Mungu wanaofanya kazi ya kusambaza Injili kupitia karama ya uimbaji,
Upendo Nkone, Ambwene Mwasongwe, Angela, Paul Clement, Martha Mwaipaja
na wengine wengi wanatarajiwa kushusha upako wa nguvu ndani ya Uwanja wa
Taifa, Agosti 8, 2014 katika Tamasha la Matumaini.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo la kila mwaka, Luqman Maloto wasanii hao watafanya shoo ya kumtukuza Mungu katika uwanja huo kama ilivyokuwa katika Tamasha la Matumaini 2013 ambapo mashabiki waliohudhuria waliburudika vya kutosha.
“Nawasihi wale wapenzi wa nyimbo za Injili waje kwa wingi kwani orodha ya wasanii inazidi kuongezeka kila siku, watakuwepo wengi kushusha upako,” alisema Maloto.
Mbali na burudani hiyo, pia kutakuwa na ‘package’ tofauti za burudani kama vile mpira wa miguu na ndondi ambapo mwaka huu Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atazichapa na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
“Tutakuwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa ambaye atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada Maugo.
“Ushindani mkali pia utawekwa na mastaa wa Bongo Movie, Cloud 112 na Jacob Steven ‘JB’ ambao siku hiyo watazipiga katika pambano la raundi nne,” alisema Maloto.
Aliongeza kuwa, mbali na mechi za mpira wa miguu kati ya Wabunge Mashabiki wa Yanga dhidi ya wenzao wa Simba, timu ya Bongo Movie itapepetana na Bongo Fleva sambamba na Azam watakaokipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

“Pia katika muziki,Yemi Alade kutoka
Nigeria atachuana vikali na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ huku wasanii
wengine wa Bongo Fleva wakiendelea kuongezeka wakiwemo Madee, R.O.M.A
Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Ali
Kiba na kwa mara ya kwanza Wema Sepetu atapanda jukwaani na kuimba
nyimbo za bebi wake Diamond,” alisema Maloto.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Sycorp na Times FM (100.5).
No comments:
Post a Comment