Stori: Imelda Mtema MWANAMITINDO
wa Bongo aliyepo nyuma ya nondo huko Macau, Hong Kong nchini China
akitumikia kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia ya kubeba
madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’
ametuma ujumbe mzito kwa mashabiki wake.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, rafiki wa karibu wa Jack
ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini, alisema kwamba mwanamitindo
huyo amekuwa akimuandikia barua mara kwa mara lakini safari hii ametaka
ujumbe wake uwafikie Watanzania.
“Amesema watu wasimhurumie kuhusu kufungwa, amesisitiza sana juu ya
suala mavazi na mitindo. Amesema hapendi kuona Tanzania inayumba katika
masuala ya mitindo ambayo yeye alikuwa akiiamini kwamba ni kazi ambayo
inaweza kuwaingizia kipato watu wengi,” alisema rafiki huyo wa karibu.
Rafiki huyo alizidi kuweka wazi kuwa mara nyingi Jack hapendi
kuwaambia juu ya maisha ya jela kwani hapendi kabisa kuwapa watu simanzi
bali anapenda watu wajue anaishi maisha ya kawaida.
“Mara nyingi Jack hapendi kabisa kueleza maisha ya jela, hapendi kuwaumiza wat, anachopenda ni kujua nini kinachoendelea katika fasheni,” alisema rafiki huyo wa Jack.
“Mara nyingi Jack hapendi kabisa kueleza maisha ya jela, hapendi kuwaumiza wat, anachopenda ni kujua nini kinachoendelea katika fasheni,” alisema rafiki huyo wa Jack.
Rafiki huyo alisema kuwa Jack bado anaagiza nguo ambazo alikuwa
akipenda kuvaa hasa lineni nyeupe na kuwataka watu wahisi kama yupo
masomoni na atarejea tu akiwa salama.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand kuelekea Guangzhou, China.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand kuelekea Guangzhou, China.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment