EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 18, 2014

JIDE, GARDNER SASA PAKA NA PANYA

Stori: Richard Bukos PAMOJA na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.
Mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ akiwa na Miss Mara 2000, Rashida Wanjara.
Tukio hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.

WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu,  baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.
JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.
WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda  kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.
‘Mtalaka’ wa Gardner, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ (kulia) akijaribu kukwepa kamera za Global.
PAKA NA PANYA!
Mtu mmoja aliyekuwa amehudhuria shughuli hiyo na mkewe, alimuita paparazi wetu na kumuuliza: “Kwani, Jide na Gardner sasa ni paka na panya?”
Mwandishi: “Kivipi?”
Mtu: “Namwona Jide yuko na kampani yake, Gardner naye na kampani yake kule. Unajua paka na panya ni vigumu kukutana! Hawa kweli hawapo sawasawa,” alisema mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Yahya.
Akaendelea: “Unajua ninavyojua mimi, Gardner ni kijana mpole sana, mwenye upendo, ila Jide ni mkali. Halafu kwa sababu yeye Jide ana pesa naamini alitaka kumpandia kichwani mumewe wakati anajua yeye ni kichwa cha nyumba. Pesa na ndoa mambo mawili tofauti.”
WAWINDWA NA KAMERA
Muda mwingi paparazi wetu aliwavizia Gardner na Rashida na kufanikiwa kuwafotoa picha kadhaa lakini kimbembe kilikuwa kwa Jide ambaye alionekana kuwa makini na kukwepa kamera ya paparazi wetu mara kadhaa huku akionekana kuwa na hasira na kuna muda meza yake iliparaganyika baada ya mwanga wa kamera kuwamulika yeye na kampani yake.
ANGALIA HII
Katika hali iliyodhihirisha wawili hao hawako sawasawa, muda f’lani Gardner aliinuka na kuelekea upande aliokaa Jide ambapo mwanamuziki huyo naye alionekana kama kutaka kukimbia na kumfanya Gardner kubadili mwelekeo wa safari yake.
Gardner akiendelea kufatilia jambo.
KUNA HII PIA
Mmoja wa mashuhuda aliyekuwa ukumbini hapo naye alimwambia paparazi wetu kuwa, aliwaona wawili hao wakikwepana baada ya kukutana kwenye njia ya kuelekea maliwatoni.
GARDNER AZUNGUMZA NA AMANI
Juzi, Amani lilimtafuta Gardner kwa njia ya simu na kumuuliza ni kwanini yeye na Jide kila mmoja aliingia ukumbini na kampani yake.Gardner: “Kaka, yeye (Jide) alikwenda pale kumpa tafu yule aliyekuwa akizindua albamu yake pale. Sasa isingekuwa rahisi tugandane pamoja kila wakati. Lakini hayo unayoniambia ni madai tu.”
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, ndoa ya wawili hao iliripotiwa kuvunjika na kila mmoja kushika njia yake huku Gardner akiwa anakanusha mara kwa mara kwamba ndoa ipo imara. Jide naye amekuwa akiweka kwenye mtandao wa Instagram picha yake yenye kidole cha pete ya ndoa bila maelezo!! Ni shiida!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate