EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, September 27, 2014

MAFUNZO YA MWEZI MMOJA YA OLIMPIKI MAALUMU TANZANIA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI YA FUNGWA RASMI

Walimu waliokuwa wakiendesha mafunzo kwa watoto hao wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Beatha Qambayot, Zilpa Masunga, Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha na Alphonsia Mwairafu.
Walimu hao wakiwa wameshika mipira ya kufundishia. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Watoto wenye ulemavu wa akili wakiwa katika picha na  wazazi, pamoja na walimu wao baada ya kumaliza mafunzo  ya mwezi mmoja ya Olimpiki Maalumu Tanzania  yaliyofikia tamati wilayani Temeke Dar es Salaam leo.
Mmoja wa wazazi akiwa na watoto hao.
Wazazi na walezi wakiwaelekeza watoto wao mchezo wa kurusha kitu na kudaka.
Wazazi na walezi wakiwaelekeza watoto wao mchezo wa kurusha kitu na kudaka.
Wazazi wakiimba pamoja na watoto wao.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wakiwaelekeza watoto hao kutembea huku wakiwa wameweka kitu kichwani bila ya kukishikilia.
Wazazi wakiwa na watoto wao kwenye mafunzo hayo.
Watoto hao wakigaiwa maputo kabla ya kuanza kuimba.
Mmoja wa watoto hao akicheza mchezo wa kupita katika ringi. Kulia na kushoto ni wakufunzi wa mafunzo hayo.
Hadija  Balila mmoja wa wazazi mwenye mtoto mlemavu  (kulia), akihojiwa na wanahabari kuhusu faida ya mafunzo hayo.
Watoto hao wakicheza mchezo wa kukimbia na kuweka mpira katika kikapu. Mchezo huo unawaandaa kuja kucheza mchezo wa kikapu.
Wakufunzi wa mchezo huo wakimtuza Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha kitenge kwa mchango wake wa hali na mali kwa kuwawezesha watoto hao kupata mafunzo hayo.
Mkufunzi Zilpa Masunga, akicheza na watoto hao.
 
Dotto Mwaibale
 
JAMII nchini imetakiwa kutowaficha watoto wenye matatizo ya akili badala yake wawashirikishe katika michezo mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa uelewa na kuimarisha viungo vyao.
 
Mwito huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Malaamu Tanzania, Frank Macha Dar es Salaam leo wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja ya olimpiki ya watoto hao kutoka wilaya ya Temeke.
 
"watoto wenye ulemavu wanapojumuika na watoto wenzao katika mafunzo ya michezo upata faraja na viungo vya miili yao ulainika hivyo kuwaongezea uwezo wa kutembea na changamka tofauti na mtoto ambaye hukosa mazoezi yatokanayo na michezo" alisema Masha.
 
Alisema mtoto anayefungiwa ndani kutokana na ulemavu wake mara nyingi anakuwa apendi kujumuika na watu wengi tofauti na mtoto ambaye anashirikishwa na wenzake katika michezo ambayo pia inawakutanisha wazazi wa watoto hao.
 
Masha alisema mafunzo hayo ya olimpiki maalumu Tanzanaia yaoanza mwanzoni mwa mwezi huu yamewashirikisha watoto 150 katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam ambap0 kwa wilaya ya Kinondoni ilifanyika Kawe, Ilala, Ukonga na Temeke katika Shule ya Msingi ya Wailes.
 
Alisema watoto walioshiriki olimpiki hiyo ni kuanzia miaka mitatu hadi nane na kuwa walikuwa wakipatiwa mafunzo ya michezo mbalimbali na walimu wenye utaalamu  wa kufundisha watoto wenye matatizo hayo ya akili.
 
Hadija  Balila mmoja wa wazazi mwenye mtoto mlemavu alisema kuwakutanisha watoto hao katika mashindano kama hayo kunawasaidia kuchangamka na kuwafanya nao wajione kama watoto wengine na akatoa mwito kwa wazazi na walezi wenye watoto wa aina hiyo wasiwafiche ndani kwa kuona aibu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate