Utu uzima dawa! Staa wa Bongo
Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi
wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza
kumlea.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo
Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani
kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume
atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza
kulea mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya
kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia
watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya/GPL
No comments:
Post a Comment